Waendesha bodaboda mnakera kulazimisha watu kupanda pikipiki zenu

kingkongtz

JF-Expert Member
Dec 28, 2019
1,018
3,447
Kwema ndugu zangu,

Bodaboda wana tabia za ajabu sana sijui kwanini.

Unaweza ukawa unatembea unashangaa wanakupigia honi.

Au upo njiani unatembea unashangaa boda huyu hapa "oya braza wapi" sasa nabaki najiuliza ina maana mimi sijui napokwenda au?

Leo nimeshuka kwenye gari akaja boda na pikipiki yake akanambia bro twenzetu kanikomalia kweli kweli, honi kibaoo nikamuuliza unajua napokwenda "akanambia we panda nikupeleke hadi ndani.

Nikaamua kupanda muda huo nishajipigia K Vant moja kichwa cheupeee. Tukaenda tumefika maeneo nikamwambia tayari nishushe. Nimeshuka tu akaomba mtonyo.

Nikashangaa nikahoji kivipi, akaongeza oya bro si nimekubeba nadai hela yangu bro.

Nikaongea nae kistaraabu, unakumbuka ulivyokuwa unanipigia honi alafu sijakuita kwahiyo mi najua umenisaidia tu.

Wakat anataka kushuka ikaja gari nikaingia ikaondoka.

Bodaboda mnakera sana na fujo zenu.
 
Unaanzia wapi kugombana na mtu muhimu namna hii?
Screenshot_20210328-230025~2.jpg
 
Ila kiukweli huwa wanaolazimisha,yaani wanafosi hela.kwani wewe haujui kuwa wapo na unawaona.
Binafsi huwa nawatuma wapokee mzigo waupeleke home basi.
Ila kupanda Bora nitembee ni njema kwa afya yangu.
Huwa ni hiace nikiwa na familia nakodi tax Ila boda napinga Sana.
Mana kwanza safety ni ndogo mno yaani mno.
Kwa wale wa traffic management watanielewa
 
Ni kweli wanatafatuta kipato na tunathamini haso zao ila sasa wamegeuka kuwa usumbufu mkubwa kwa watembea kwa miguu hasa vituoni mtu anaposhuka kwenye gari.
 
Kweli wana kera ila ndio njia zao za kupata riziki
Yaani wao kila mahali ni kijiwe tu na anaona huenda unaelekea kupanda bado na hapo anaona akuwahi

Hawa wana target ya kutengeneza kiasi flani cha hela kwa wiki
Ndio maana wanapambana hivyo
Wachukulieni poa tu na maisha yaende
Au tuwaongezee kodi ya Uzalendo
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom