Waenda kufunga ndoa kwa bodaboda, warudi kwa miguu

May 8, 2013
40
6
WAENDA KUFUNGA NDOA KWA BODABODA, WARUDI KWA MIGUU

by GLOBAL
WANANDOA Charles Kanyema (29) na Bi. Onoratha Pascal (28) hivi karubuni waliwashangaza wakazi wa Manispaa ya Morogoro baada ya kwenda kufunga ndoa wakiwa wamepanda bodaboda na kurejea nyumbani kwa kutembea kwa miguu.
Ndoa hiyo iliyofungwa katika Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Mjini na kufungishwa na Paroko Msaidizi, Padri Phidelisi Mwesongo iligharimu shilingi 45,000 tu.
“Gharama hizo ni pamoja na picha 5 kwa ajili ya kumbukumbu yetu na nyumbani tumenunua mchele na nyama kwa ajili ya sherehe ndogo,” alisema bwana harusi Kanyema.
Alisema fedha hizo zilitokana na michango waliyochangiwa na wana jumuiya wenzao na hawakutaka mambo makubwa katika sherehe yao.
Mara baada ya kuwafungisha ndoa, Padri Mwesongo aliwataka wanandoa hao kutambua kwamba maisha ya ndoa ni magumu na yanahitaji uvumilivu ili ndoa yao iweze kudumu.
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe hiyo waliwasifu wanandoa hao kwa kutotumia gharama kubwa wakidai kwamba mara nyingi ndoa zilizojaa kila aina ya mbwembwe huwa hazidumu
 
Jamii ya Tanzania inafaa kuiga mfano huo ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili.Unakuta mtu anataka harusi kubwa halafu anategemea kuombaomba michango kama omba omba.Kwa nini usifanye harusi ya kawaida kulingana na uwezo wako.Jitu linapanga budget ya milioni 20 wakati halina hata kiwanja sasa huo si uzezeta.Tena wengi wao ni wasomi kabisa.Watanzania badilikeni acheni tabia ya kuombaomba michango ya harusi huo si utamaduni wetu.

Mababu zetu walikuwa wanachinja ng'ombe wanaalika wanandugu na majirani wanasherehekea na bibi harusi anaagwa mchezo unaishia hapo huo ndio utamaduni wetu.
 
Back
Top Bottom