Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

Dah umenikumbimusha mbali sana. Pilau linapikwa mara 2 kwa mwaka na likipikwa wanaalikwa ndugu.

Wali ulitumia masaa 7 kupikwa maji yanachemshwa, nazi inakunwa moto unawekwa juu ya sinia.

Mgeni akija wa heshima jogoo anachinjwa.

Picha inapigwa huku umejipaka mafuta na kuweka dole.

Ligi za soka za mtaa, na mpira ukiisha ni ngumi mpaka apatikane mbabe wa mtaa.

Picha inapigwa kijijini kuipata ni baada ya mwezi, mpaka mpiga picha akaoshe picha mjini/studio.

Santuri ndio zinatumika, sahani kubwa nyimbo 3
 
Ukiachana na haya ya album, hivi hawa watoto waliozaliwa juzi juzi wanajua kwamba hawa tunaowaita wapiga debe jina lilitokana na kitu flani cha pembe nne kinachioitwa debe? Waliwahi kuliona debe? Siku hizi yapo wapi madebe wahenga?
Yale madebe yaliandikwa Korie, palikuwa na picha ya mwanaume aliyevalia nguo na kofia nyeupe(mavazi ya wapishi)
 
Ampate wapi mpiga picha wakati tablet mama yake anayo palepale?
Kiza kitakosa kumbukumbu hiki haa enzi hizo mpiga picha anabaiskeli yake ya swala.

Usidahau kuwaambia picha za enzi hizo zilikuwa na kitu kinaitwa negative hii ndio inatoa nakala ya picha, na zilikuwa zinaibwa saana mtu akipenda picha katika album.
 
Mikanda mizuri ilikuwa ni Kodak na konica
images%20(1).jpg
images.jpg
 
Dah, miaka ya 99 kipindi hcho nimeenda chuo mkoani yaani kila mgeni atayekuja anatolewa album yangu na nyingine za nyumbani,utasikia hyu ni mwanangu wa pili anasoma chuo huko mkoani,jamn karibia kila mgeni anaondoka na picha yangu mpaka nkawa najiuliza hivi mama yangu ananitakia nini
Mama yako alikuwa anakupenda sana mkuu
 
Wale wa kijijini tulikua tunasubiri hadi mpiga picha ajaze mkanda ndo aende mjini kusafisha. Usiombe iwe sio msimu wa sikukuu maana wateja wachache afu baada ya mwezi mzima anakuja picha imeungua😆😆.
Those were the days
 
Wa miaka hii wangekua wanachomoa picha na kuzipost Kwa Social Media, unajiuriza nani kaiba picha langu? Na wangefanyia kwa Photoshop ushangae
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom