Wadhamini wote wa mpira nchini wanazilenga Simba na Yanga, TFF lifahamu hilo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Kila mtu, kampuni au taasisi yoyote inayodhamini timu yoyote inayoshiriki LigiKuu inafanya hivyo kwa kuzilenga Simba na Yanga ziwape faida kwenye biashara zao. Hata yule atakaetoa udhamini kwa timu ndogo kama Geita Gold lengo lake ni simba na yanga wamtangaze siku kitimu hicho kitakapocheza mechi zake na Simba na Yanga. Huu ni ukweli ambao TFF lazima iutambue itake isitake.

Hata NBC, GSM, Azam Media na TBC walikubali kutoa udhamini kwa kuzitegemea simba na yanga kupata faida. Hata timu nyingine zote kwenye ligi zinazitegemea Simba na Yanga kupata faida kwenye viingilio viwanjani.

Hata TFF inazitegemea Simba na Yanga kupata mapato (wadhamini, viingilio) ya kuendeshea mpira nchini; hivyo hivyo na serikali inazitegemea Simba na Yanga kupata kodi na wachezaji kwenye timu yake ya Taifa.

Ukweli huu ndio unaosababisha timu za ligi ya kwanza na ligi ya pili hazipati wadhamini kwakuwa hazina mechi na Simba na Yanga.

Kwa sababu hivyo hakuna namna yoyote ile TFF itakavyoweza kuzitambuka Simba na Yanga wakati wa kuingia mikataba ya udhamini wa aina yoyote ile bila kuzishirikisha kikamilifu Simba na Yanga.

TFF imekosa, imekosea na imekosa sana kuingia mikataba ya udhamini bila kupata maoni ya hizi timu mbili ingawa katiba ya TFF inaondoa umuhimu wa kuzialika timu kwenye uingiaji mikataba.

Makosa haya yamesababisha Yanga kugomea rangi ya logo ya NBC na Simba kugomea udhamini wa GSM after the fact.

Kwavyovyote vile GSM isingeendelea na mkataba ule bila uwepo wa Simba na Yanga pamoja.

Simba na Yanga zinatumia gharama nyingi sana za kiuendashaji ili kuifanya ligi ionekane kama inavyoonekana sasa, sio timu za kuswaga tu sawa na Ruvu shooting, Namungo au Ihefu.
 
Kama GSM lengo lake lilikuwa Simba angeacha kelele za kuidharau Simba pia asingekuwa KIT maker wa Yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida hapo ni TFF sio GSM, Ibara ya 77 ya katiba ya tff inaipa TFF mamlaka ya kuingia makubaliono na mdhamini bila kuzialika timu. Na bahati mbaya sana katiba hii ilipita bila kupingwa na vilabu vyote. Sasa hivi ndio wanaishtukia, lakini it is too late. Kwahiyo kwa mujibu wa Katiba ya TFF timu zimulize TFF kuhusu haki zao, sio GSM.
 
Back
Top Bottom