Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kwamwewe, Oct 26, 2010.

 1. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo


  James Magai

  MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Ijumaa iliyopita iliwasweka mahabusu siku 14 wadhamini wawili wa mshtakiwa baada ya kuingia mahakamani wakiwa katika hali ambayo mahakama hiyo iliitafsiri kuwa ni nusu uchi.

  Kabla ya mahakama hiyo kuamuru waswekwe rumande mwishoni ,wadhamini hao Ramadhani Bakire (19) na Mgeni Jetta (22) walifika mahakamani hapo kwa lengo la kumuwekea dhamana ndugu yao anayekabiliwa na kesi ya jinai.
  Wakati wakiingia mahakamani hapo walikuwa wamevalia suruali aina ya Jeans wakiwa wamezifunga kwa mikanda chini ya makalio katika mtindo uitwao "kata k" huku nguo za ndani zikionekana hadharani.

  Hakimu Wilberforce Luhwago aliyekuwa akisikiliza kesi ya ndugu yao huyo alilazimika kuacha kusoma barua zao hizo za udhamini baada ya kuona nguo zao za ndani zikiwa nje hadharani ndani ya mahakama na kuwahoji sababu ya kuingia mahakamani wakiwa wamevaa namna ile.

  "Ninyi kwa nini mnaingia mahakamani mkiwa mvaa nguo huku mmezishusha namna hiyo?" alihoji Hakimu Luhwago.

  "Mheshimiwa Hakimu, kosa la kwanza si kosa tusamehe tu na siku nyingine hututakuja hivi," alijibu mmoja wa wadhani hao, Ramadhani Bakire huku akipandisha suruali yake baada ya kubaini Hakimu kutopendezewa na hali.

  Hata hivyo licha ya utetezi wao huo, Hakimu Luhwago aliyeonekana kukerwa na hali hiyo aliwaambia kuwa kamwe hawezi kuruhusu Mahakama kugeuka kuwa uwanja wa kufanyia maigizo na kwamba karipio la mdomo pekee halitoshi isipokuwa kuwapumzisha rumande

  "Siwezi kuwapa karipio la mdomo kama njia ya kuwafundisha jinsi ya kuingia Mahakamani kwa adabu.Nafikiri aina ya uvaaji mliouvaa umeanza kukubalika kwa baadhi ya macho ya watu na katika baadhi ya maeneo fulani fulani;

  Lakini kwa hakika siwezi nikaruhusu na Mahakama nayo kuwa sehemu inayoweza kuvaliwa uvaaji wa aina hii, huu ni uhuni. Kwa hiyo mtapumzika ndani (mahabusu ) hadi kesi hii itakapotajwa tena hapa mahakamani (Novemba 5 mwaka huu)" alisema Hakimu Luhwago.

  Mwanamke mmoja aliyejiambulisha kwa Hakimu huyo ni dada wa vijana wadhamini hao alimuomba hakimu huyo awasamehe kwa kosa hilo, lakini bila mafanikio.

  "Umeshindwa kuwalea na kuwafudisha kuwa aina ya uvaaji huo una mipaka, najua kazi ya malezi ni ngumu, na hata viongozi wa dini hawajafanikiwa sana katika hilo;

  Kwa hiyo ndio maana sasa Mahakama inasaidia ulezi huo angalau kwa siku 14 tu hawatahitaji kufunzwa tena na hawatorudia tena kuingia kihuni mahakamani," alisisitiza Hakmu Luhwago.
   
 2. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Huyu aliwaonea hawa jamaa.
  hakuna mahali palipotoa angalizo la mavazi ya heshima au la!
  Ana lake jambo.......
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mahakimu wetu hao wako very emotional kwenye kufanya maamuzi..
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  nadhani ni chadema huyu
   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mi nakubaliana naye tu huyu Hakimu. Vijana wanatutia aibu sana wawe wa kiume au wa kike uvaaji mwingine hauna tija kabisa.
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana,maana kuna baadhi ya wanaume,wanazalilisha utu wa mwanaume na binadamu kwa ujumla.Na ikumbukwe si kila sehemu ni sehemu ya kufanya mzaha!mahakamani si ukumbi wa disco au vijiweni!
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Dressing code ya mahakamani kwa raia ni ipi ? nsijefungwa miye kasho naenda kutoa ushaidi huko
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  safi sana hii kitu.

  Mbona huko mnakoiga na wao wanawekwa ndani watu? Hebu vaa hivi baadhi ya miji USA uone moto.

  Wala si lazima Mahakamani, hii hata mtaani, wakikuona, wewe umekwenda.  Are Your Jeans Sagging? Go Directly to Jail.

  http://www.nytimes.com/2007/08/30/fashion/30baggy.html
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuwa Masikini sana, ila Hakimu ataona kwa jinsi gani umejitahidi KUVAA KWA HESHIMA.

  Huwezi kuvaa JEANS nzuri, kila kitu safi na unaacha Mata*o yako nje ndani ya Mahakama.

  Hata dada zetu wakiwa Club, wanavaa ovyo ila wakitoka nje, wanaweka khanga.

   
 10. bona

  bona JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  nadhan angewakatalia kutomdhamini ndugu yao ingetosha kwani wangepata fundisho kua wamemponza ndugu yao! ila wiki mbili naona kama ndefu sana!
   
 11. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mmhh!!
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Ni kweli vijana wamekosea kwa uvaaji wao, lakini naona kama hakimu hakutenda haki kwa hao vijana,, angalau angewapa onyo au hata kuwaweka ndani kwa masaa machache au siku moja ingetosha kabisa kuwapa funzo...
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Aaah jamani, wiki mbili wakae ndani si mchezo.
  Kama vipi mahakama zibandike matangazo ya "usivae kata k" kama ambavyo ofisi nyingi zina matangazo ya "no smoking".
   
Loading...