Wadhamini wamwandikia barua Mbowe kumtaka Lissu arejee Tanzania

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,797
Dar es Salaam. Wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania kuwa juhudi walizofanya kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani ni pamoja na kumwandikia barua Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Mdhamini huyo Robert Katula amedai hayo leo Jumatatu Januari 20,2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Lissu ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi yuko nchini Ubelgiji alikokwenda kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa kwenye makazi yake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.

Desemba 19, 2019 Mahakama hiyo ilitoa amri kwa wadhamini hao kuhakikisha mshtakiwa huyo anafika mahakamani.

"Tumefanya juhudi ya kuwasiliana na mshtakiwa akasema anawasiliana na wakili wa chama baada ya hapo akawa kimya, tukalazimika kumwandikia Mbowe barua kwa kuwa ndiye aliyemtoa nje ya nchi," amedai Katula

"Wakati natoa ahadi ya kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani sikujua kama atapigwa risasi lakini juhudi tulizofanya ikiwa ni kuwasiliana na mwenyekiti wake zinaweza kuzaa matunda," amedai

Mdhamini huyo amewasilisha nakala ya barua aliyomwandikia Mbowe na kudai akishafika nchini Tanzania anaweza kumleta mahakamani.

Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto ameeleza jukumu la mdhamini ni kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani ni la mdhamini mwenyewe.

"Wadhamini hawa walikubali kumwekea dhamana na kuridhia kama ni kujitoa wangejitoa kabla mshtakiwa hajaenda nje ya nchi," amedai Mitanto

Hakimu Simba amewataka wadhamini hao kuhakikisha mshtakiwa analetwa mahakamani kabla mahakama hiyo haijatoa amri nyingine.

"Usifikiri tutakusamehe jukumu lako ndilo hilohilo mtuletee mshtakiwa kwa kuwa jalada hili halijui hofu, huo ndio mkataba wako," ameeleza Hakimu Simba

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 20, 2020 itakapotajwa tena.

Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Mbali na Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati Januari 12 na 14, 2016 jijini Dar es Salaam, ambapo Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi.
 
Kweli mkuu nmepata updates kutoka kwa millardAyo....

Hapa ndpo mtaamini tuna mahakama zetu zmejaa vitisho tu.....
"Et kabla hatujatoa maamuzi magumu,kwani hayo maamuzi hayapo kwenye Sheria??? By the way Chadema toka lini wanahtaji maamuzi yasiyo magumu?
Ningekuwa mdhamini wake na Lissu wangetoa tu
Mimi Kama mdhamini niljua Kama Lissu atakuja kupgwa risasi????
Sijui hayo maamuzi magumu ni yapi... Ngoja nikohoe kwanza
 
WADHAMINI wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamemwandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakimuomba awasaidie kumleta mshitakiwa Lissu hapa nchini.

Mdhamini Robert Katula ameeleza hayo leo Januari 20, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa ambapo amedai, wamefanya juhudi za kuwasiliana na mshitakiwa ambapo mara ya mwisho aliwaeleza kuwa anawasiliana na Wakili wa chama chake.

Hata hivyo, licha ya wadhamini kudai kuandika barua Mahakama imeendelea kusisitiza kuwa inamuhitaji Lissu mahakamani hapo ili shauri linalomkabili yeye na wenzake wanne liweze kuendelea katika hatua nyingine.

Akiendelea kueleza wakili Katula amedai pamoja na mshtakiwa kuwaeleza hivyo, mpaka leo hawajafanikiwa kupata jibu lolote ndipo walipoamua kumuandikia barua Mbowe ili awasaidie kumleta mshitakiwa huyo nchini ili waweze kumfikisha mahakamani kwani wakati tunamdhamini Lissu hatukujua kama atapigwa risasi na kuondoka hapa nchini,.

"Mheshimiwa, tumemuandikia barua Mwenyekiti wa chama chake ili atusaidie kumleta hapa nchini mshtakiwa na sisi tuweze kumleta mahakamani hivyo tunaomba muda zaidi wa kufatilia majibu ya barua hiyo," ameeleza Katula.

Akijibu hoja hizo, wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto alidai kuwa ni jukumu la wadhamini kuhakikisha mtuhumiwa anafika mahakamani na si la mtu mwingine na kwamba wadhamini hao walikubali kumuwekea dhamana mshitakiwa huyo hata kabla ya kuugua na walilidhia asafiri na kuongeza kuwa walikuwa wanajukumu la kujitoa katika nafasi hiyo kabla Lissu hajasafiri.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema kuwa suala bado linabaki pale pale kuwa mshitakiwa huyo aletwe mahakamani kwani kupigwa kwake risasi hakumzuii kufika mahakamani na kuhudhuri kesi yake.

Tunaomba mtuletee mshitakiwa hapa, tena (mdhamini) usije ukafikiri tutakusamehe tunakupa muda mwingine tuletee mtu huyo kabla atujatoa amri nyingine itakayokuwa ngumu zaidi dhidi yenu wadhamini na mshitakiwa mwenyewe," amesema Hakimu Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 20, 2020 na kusisitiza Lissu kufika mahakamani na kwamba dhamana kwa washitakiwa wengine inaendelea

Mbali na Lissu washitakiwa wengine ni Mkina, Mhariri wa gazeti la Mawio, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Lissu na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria
 
Kwani mahakama si pia hutoa maamuzi hata kama mtuhumiwa hayupo mahakamani,kinachowashinda ni nini kama wanaamini alifanya kosa?
 
Hizi Picha kuna yule Mzee zimemchanganya kabisa
tapatalk_1579539026704.jpg
tapatalk_1579539021902.jpg


Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom