Wadhamini wa Watuhumiwa wa uhujumu uchumi mtegoni

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Watuhumiwa wanne ambao wameshtakiwa na kesi ya uhujumu uchumi wanaendelea kusota katika mahabusu ya gereza kuu la Kisongo kwa zaidi ya miezi kumi wakati dhamana yao iko lakini kila wadhamini wanapojitokeza kuwadhamini watuhumiwa hao hujikuta wakikamatwa na Polisi wa kituo Kikuu cha polisi Arusha kwa kupigwa,kuteswa na kunyang'anywa mali walizokuwa nazo ikiwemo simu,pesa na vitu vya thamani bila sababu za msingi.

Watuhumiwa hao ni Stephen Mhando (32) mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam, Yunus Hamed (37) wa Korogwe, Tanga Said Hamisi (38,)mkazi wa Kariakoo, Dar es Salaam na Msafiri Yohana (22) aliyedaiwa kuwa mganga wa kienyeji mkazi wa Magu Mkoani Mwanza.

Wote hao walikamatwa kati ya Mei 3 na 4 mwaka jana na Mei 7 aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ausha, Jonathan Shana alitangaza kuwa wamekamatwa Daraja la Nduruma wakijiandaa kwenda kufanya ujambzi Mkoani Arusha.

Katika tangazo hilo alolilotoa mbele ya Waandishi wa Habari, Shana ambaye kwa sasa ni marehemu,alisema kuwa watuhumiwa hao walikuwa katika gari aina ya Toyota Crown lenye namba za usajili T777 DSJ wakiwa na nia ovu ya kufanya ujambazi.

Hata hivyo, Mei 8, 2020 watuhumiwa hao walipofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa mbele ya Hakimu Mfawidhi Martha Mahumbuga,walisomewa shtaka moja la uhujumu uchumi katika kesi namba 39/2020 ambayo dhamana yake ilikuwa wazi ambayo ni wadhamini wawili, mmoja akiwa mtumishi wa serikali.

Katika hatua isiyokuwa ya kawaida wadhamini wote waliojitokeza,walikamatwa na Polisi kila wanapofika mahakamani, walitishiwa kuteswa na hata kuuwawa bila sababu zozote kuelezwa wadhamini.

Mmoja wa wadhamini hao ambaye ni mtumishi wa serikali na jina lake linahifadhiwa kwa sasa, alidai kuwa alikamatwa alipofika mahakamani kumdhamini mmoja wa watuhumiwa lakini aliishia kukaa mahabusu kwa siku saba katika kituo kikuu cha Polisi Jijini hapa.

“Mimi ni mtumishi wa umma, nilifuata taratbu zote za kumwekea dhamana mmoja wa watuhumiwa lakini niliishia kukaa rumande siku saba kwa amri ya kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi Arusha bila sababu zozote.

“Katika umri wangu,sikuwahi kutegemea vitisho,kebehi na kejeli zilizokuwa zinatolewa na huyo kigogo hapo central.na kamwe sina hamu ya kufika hapo wala mahakamani kumsaidia ndugu yangu ambaye naamini si jambazi,’’ alisisitiza Mtumishi huyo.

Alidai kuwa wadhamini waliofika kuwawekea dhamana iliyo wazi katika shauri hiyo wamekamatwa mara tatu na wamekamata tamaa ya kufika hata mahakamani wakiogopa kutiwa mbaroni na wanamwomba Rais Magufuli awasaidie ili ndugu zao waweze kudhaminiwa.

Hata hivyo Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Arusha Hakimu Mahumbuga yeye alisema mbele ya mahakama wakati watuhumiwa wakiwasilisha malalamiko juu ya hali hiyo alikiri kuwa dhamana iko wazi na yeye ametimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria ya kuwadhamini ila hayo ya wadhamini kukamatwa hana taarifa nayo na kuuliza kwa nini wanakamatwa lakini hakuna majibu kutoka kwa mwendesha mashtaka wa serikali.

Hakimu alisikika kusema tena kuwa dhamana iko wazi kwa watuhumiwa wote na kama wadhamini wako taratibu zote zifuatwe ili kila mmoja atimize wajibu wake wa kisheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alipoulizwa juu ya polisi kukamata wadhamni na kuwaweka rumande na kuwatesa ka kipigo alisema kuwa yeye hana taarifa juu ya hilo ila aliahidi kulifuatilia hilo.

Masejo alisema atafuatilia kwa ukaribu juu wadhamini kukamatwa na polisi ili kujua utata ulipo na kutolea ufafanuzi.

Mwisho.
 
Kosa mbele ya media jingine mahakamani linatajwa jingine.

Nilifanya kosa la kugoma kusachiwa kituoni nikaandikiwa kosa la kuvunja na kuiba.

Askari ndivyo walivyo
 
Polisi ni washenzi sana kesi kama hizi ndio zinafanya watanzania wengi kuichukia hii awamu. Ni udhalimu kila mahala.

Kuna haja ya kuundwa tume ya kuchunguza kesi zote zilizofunguliwa za Uhujumu uchumi nina hakika nyingi ni za kubambikiwa na polisi
 
Back
Top Bottom