Wadhamini wa Simba FC Bia ya Kilimanjaro wajiondoa Simba,kisa ni gogoro!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Kufuatia Klabu ya Simba kukubwa na mgogoro mkubwa huku mwenyekiti wake mh Ismail Aden Rage aka TUTU VENGERE akiigomea TFF kuitisha mkutano wa kutafuta suluhu,leo wadhamini wa klabu hiyo wametangaza kujiondoa kuidhamini klabu hiyo kwa kusema kwamba wao wanadhamini mpira na siyo ngumi.
Wakati huo huo rais wa TFF mh J Malinzi ametangaza kwamba kutakua na kikao cha kamati ya utendaji siku ya tar 22.dec.013 kikiwa na lengo la kujadili vurugu zinazoendelea ktk klabu ya Simba.
Naomba kuwasilisha.
 
Ingawa Mkuu mandieta hujatoa source, naunga mkono hoja kwa 100% wadhamini kujitoa ili liwe fundisho si kwa wengine tu bali hata kwa viongozi wenye rageism wanaokataa kuheshimu katiba na maamuzi ya walio wengi.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Makoye Matale chanzo cha habari ni J.Malinzi kupitia magic fm
 
Last edited by a moderator:
Sawa, ila ingekuwa vyema iwapo kabla ya kujiondoa, wadhamini wangejaribu kukaa na pande zote mbili kujaribu kusuluhisha. Hata kama wangeshindwa kusuluhisha, angalau wangepata upeo wa kujua nani hasa ni mkorofi kati ya pande zinazovutana. Huenda hukumu hii ya wadhamini ni sawa na kuwaadhibu pia wasiohusika na mgogoro huo.
 
kwanza warudishe mamilioni ya wadau waliochanga kupitia shindano la nani mtani jembe, wasilete janja ya kutokomea na hela za wanachama!!
then hao kilimanjaro wajue Simba ilikuwepo hata kabla bia ya kilimanjaro haijaanza kuzalishwa
serengeti wapo tena ndo itakuwa tamu, kule TBL kwetu SBL
 
Kufuatia Klabu ya Simba kukubwa na mgogoro mkubwa huku mwenyekiti wake mh Ismail Aden Rage aka TUTU VENGERE akiigomea TFF kuitisha mkutano wa kutafuta suluhu,leo wadhamini wa klabu hiyo wametangaza kujiondoa kuidhamini klabu hiyo kwa kusema kwamba wao wanadhamini mpira na siyo ngumi.
Wakati huo huo rais wa TFF mh J Malinzi ametangaza kwamba kutakua na kikao cha kamati ya utendaji siku ya tar 22.dec.013 kikiwa na lengo la kujadili vurugu zinazoendelea ktk klabu ya Simba.
Naomba kuwasilisha.

Acha Mambo Ya Kike na Ya Kishoga na Upotoshaji na Wadhamini Hawajajitoa Kama Usemavyo bali Wameitaka Klabu Yetu Ikae Chini na Imalize Mgogoro Wake la Sivyo Wanaweza Wakafikiria Kujitoa. Siyo Kila Mtu ni MJINGA na -------- kama Ulivyo na Najua Wewe Utakuwa ni GONGO WAZI KANDAMBILI. Vipi Ziara Yenu Ya Kupeleka POWDER UTURUKI imefikia Wapi? MNATAKA MFIDIE HASARA MLIYOIPATA KTK KUENDESHA Timu? Na Safari hii Mkienda tu Na Powder na Mkichukuwa Powder MNAUMBUKA na TIMU NZIMA itanyongwa Mtutie Hasara na Aibu Taifa Letu.
 
Wadhanimi waliingia kwa mkataba unless kama kuna kipengele cha kujiondoa kinachoendana na hoja zao
 
Sawa, ila ingekuwa vyema iwapo kabla ya kujiondoa, wadhamini wangejaribu kukaa na pande zote mbili kujaribu kusuluhisha. Hata kama wangeshindwa kusuluhisha, angalau wangepata upeo wa kujua nani hasa ni mkorofi kati ya pande zinazovutana. Huenda hukumu hii ya wadhamini ni sawa na kuwaadhibu pia wasiohusika na mgogoro huo.
Hivi inaingia akilini mtu kukupa pesa za kutatulia matatizo yako alafu achukue na kazi nyingine ya kukusuluhisha!? Itakuwa ni Tz pekee duniani.

Kwani kazi ya wadhamini ni kutatua migogoro?
 
1. Madhumuni mamojawapo ya udhamini wa soka ni kuitatulia timu husika matatizo yake (ukosefu wa rasilmali, n.k.) ili timu hiyo ifanye vizuri na hivyo kuitangaza shughuli ya mdhamini. Kwa kuwa matatizo hayana mipaka, si vibaya kusaidia hata hilo tatizo la uongozi kutoelewana. Si lazima, lakini ni vyema.
2. Tayari mdhamini huyo ameshawekeza mamilioni ya fedha kwa timu hiyo. Kimahesabu (na kihesabati), ni nafuu zaidi kusaidia kutatua mgogoro huo kuliko kuanza na timu mpya ambayo bila ya shaka haina tija kiudhamini kuliko ilivyo Simba.
 
Hivi inaingia akilini mtu kukupa pesa za kutatulia matatizo yako alafu achukue na kazi nyingine ya kukusuluhisha!? Itakuwa ni Tz pekee duniani.
Nadhani inaingia sana akilini, maana kama ulivyosema mdhamini ameipa pesa Simba za kutatulia matatizo yake. Sasa linapojitokeza tatizo lisilohitaji fedha kulitatua, kwa nini mdhamini asijaribu kusaidia? Mathalani ukinipa hela ya mahari nikaolea, haitaingia akilini kuniketisha kitako na niliyemwolea pesa hiyo pale ndoa yetu inapoyumba sababu ya wawili sisi kutoelewana?
 
Naona hatutaelewana...

1. Madhumuni mamojawapo ya udhamini wa soka ni kuitatulia timu husika matatizo yake (ukosefu wa rasilmali, n.k.) ili timu hiyo ifanye vizuri na hivyo kuitangaza shughuli ya mdhamini. Kwa kuwa matatizo hayana mipaka, si vibaya kusaidia hata hilo tatizo la uongozi kutoelewana. Si lazima, lakini ni vyema.
2. Tayari mdhamini huyo ameshawekeza mamilioni ya fedha kwa timu hiyo. Kimahesabu (na kihesabati), ni nafuu zaidi kusaidia kutatua mgogoro huo kuliko kuanza na timu mpya ambayo bila ya shaka haina tija kiudhamini kuliko ilivyo Simba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom