Wadau, wasomi wakosoa matokeo ya kidato cha nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau, wasomi wakosoa matokeo ya kidato cha nne

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Feb 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Elimui na Mafunzo ya ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa.


  Baadhi ya wasomi na wadau wametoa maoni kuhusu matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne wa mwaka 2011, ambao matokeo yake yalitangazwa juzi na Baraza la taifa la mitihani (Necta).

  Profesa Mwajabu Posssi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema serikali inapaswa kutambua kuwa umasikini unaokabili familia nyingi za kitanzania ndiyo sababu ya wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao na badala yake wazazi wanatumia muda mwingi kutafuta kipato kukithi hali ya maisha ya sasa.

  Profesa Posssi alisema familia nyingi za sasa zinajihusisha zaidi na utafutaji pesa na kukosa muda wa kufuatilia maendeleo ya elimu kwa watoto wao.

  “Imekuwa kawaida kwa mzazi akimpeleka shule mtoto humwachia mwalimu moja kwa moja na hii inatokana na kupanda kwa gharama za maisha,” alisema Profesa Possi.

  Waziri wa zamani wa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai, amesema matokeo mabaya ya ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne ni matunda ya kufuta kisiasa maboresho yaliyofanywa na timu za wataalamu katika sekta ya elimu.

  Alisema mojawapo ya mambo yaliyofanywa kisiasa na kuliingiza taifa katika hali mbaya ya kushuka kwa kiwango cha elimu nchini na hatimaye kulifanya taifa kukumbwa na maafa hayo inatokana na kuifuta mitihani ya kidato cha pili miaka iliyopita kwa maslahi ya kisiasa.

  Mungai alisema ingawa serikali imerejesha mtihani huo ili kukabiliana na ufaulu mdogo, maboresho yote ya kitaalamu yanayofanywa kwa kuzingatia tafiti ziheshimiwe na zisiingiliwe na wanasiasa ili kumaliza udhaifu huo.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udomasa), Paul Loisulie, alisema matokeo mabovu kwa wanafunzi wa kidato hicho yanatokana na walimu kutopewa kipaumbele na serikali.

  Alisema kuwa matokeo hayo mabaya ni matunda ya serikali kutowajari walimu na kuwacha wakiwa katika mazingira magumu hivyo kushindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  Aliongeza hali hiyoitaendelea kuigarimu serikali na kutangaza matokeo mabovu.
  Alisema kuwa kama serikali inataka kuepukana na hali hii, haina budi kuwajengea uchumi imara walimu ambao utapunguza manung’uniko.

  Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi, Padri Wiliam Ruahich, alisema matokeo mabaya yanasababishwa na mambo kadhaa, likiwemo suala la uongozi mbovu kwa baadhi ya shule.

  Alisema shule nyingi hazina walimu wa masomo ya Sayansi ambayo wanafunzi wengi wameanguka kwa kupata alama za chini.

  Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mwenge, Profesa Donge, alisema serikali haina budi kukaa chini na kutafakari juu ya hali ya matokeo hayo ikiwemo kuangalia njia zitakazowasaidia walimu kufundisha
  kwa moyo kwa kuwapatia motisha kulingana na masomo wanayofundisha

  Alisema walimu pia hawana budi kuboreshewa mazingira ya kufundishia kwa kupewa vitendea kazi kwa shule zao za kata.

  Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Changombe, Dk. Joviter Katabaro, amesema matokeo mabaya ya kidato nne mwaka 2011 yametokana na maandalizi mabovu wanayopata wanafunzi kuanzia shule za msingi pamoja na uhaba wa vifaa vya kufundishia.

  Alisema kuwa shule za sekondari za binafsi zimeongoza kwa kuwa zinafanya maandalizi mazuri pamoja na walimu wao kuwa na moyo wa kufundisha.

  Alisema kuna sababu nyingi zilizochangia matokero mabovu zikiwemo za walimu wa shule za serikali kuvunjika moyo wa kufundisha kutokana na kufanya kazi katika mazingira magumu.

  Alitaja sababu zingine kuwa ni wanafunzi wa shule za sekondari za serikali wanakuwa hawana msingi mzuri tangu wanapokuwa shule za msingi na wanapoingia sekondari pia wanakuta mazingira ya kujifunzia mabaya.

  Aliongeza kuwa shule za sekondari za binafsi zinafanya vizuri kutokana na kuwa na walimu wenye moyo wa kufundisha pamoja na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kujifunzia.

  “Shule za serikali walimu wake hawana moyo wa kufundisha kutokana na madai yao mbalimbali kupuuzwa, lakini pia wanafunzi wengi wa shule za sekondari za serikali wanafundishwa kwa kukariri,” alisema.

  Aliongeza kuwa ili kumaliza tatizo la wanafunzi kufeli mitihani kwa shule za serikali ni lazima hatua kadhaa zichukuliwe zikiwemo za kuongeza vifaa vya kufundishia na serikali kuwalipa walimu maslahi mazuri.

  Imeandikwa ka Emmanuel Kimweri, Richard Makore, Samson Fildolin, Ninaeli Masaki,Dar; Godfrey Mushi, Iringa; Paul Mabeja, Dodoma na Charles Lyimo, Moshi.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tatizo ni mfumo wa elimu umeharibiwa na wanasiasi.mimi ni mwalimu wa sekondari unakuta kidato cha tatu mwanafunzi hajui kusoma wala kuandika.amepita kote mpaka hapo bila kikwazo.kidato cha 4 mtihani lazima aandike bongo fleva.
   
 3. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwa nini watoto wengi wanaoingia sekondari zetu za kata wanakuwa weupe kiakili wakati wanakuwa wamefauli mtihani wa darasa la saba. Shule za msingi kwa sasa hakuna taaluma kama zamani ni bora liende wanafunzi wanapewa njia za kuibia mtihani tu ndio maana udanganyifu unazidi kila mithani
   
Loading...