Wadau waiponda bajeti Wizara ya Elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau waiponda bajeti Wizara ya Elimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 14, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu nchini, wameiponda bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuwa imeshindwa kuonyesha njia ya kutatua changamoto zinazoikabili.

  Chama hicho, kimesema kimesikitishwa na hatua ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, kushindwa kuzungumzia mgogoro wa walimu na Serikali.

  Wakizungumza mjini Dar es Salaam jana katika mdahalo wa bajeti ya wizara hiyo, ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Kuondoa Umaskini (REPOA) na Hakielimu, walisema bajeti hiyo inaendelea kukandamiza walimu.

  Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema katika bajeti hiyo hakuna jambo lolote jipya ambalo linaashiria kutatua mgogoro wao dhidi ya Serikali.

  “Kwanza tumesikitishwa sana na kitendo cha waziri kukaa kimya na kuacha kuuzungumzia mgomo wetu, ameashiria kuendelea kuweka msimamo wake kama alivyowahi kusema hapo awali kuwa serikali haina mgogoro na walimu.

  “Pia imeendelea kuweka kipaumbele katika matumizi ya kawaida zaidi badala ya matumizi ya maendeleo, hatuwezi kuendelea kutegemea miujiza kuboresha elimu nchini.

  “Kwa hali hiyo, mgogoro huu utaendelea kuzidi, kwani ni sawa na kuweka mafuta ya petroli kwenye moto,” alisema.

  Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Kitila Mkumbo, alisema bajeti hiyo haikujikita katika kutatua tatizo la migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

  “Zaidi ya asilimia 80 ya migomo na migogoro ya vyuo vikuu, inasababishwa na mfumo mbovu wa bodi ya mikopo.

  “Katika hili utatuzi wake serikali inapaswa kubadilisha kabisa mfumo huu wa utoaji mikopo na si kuongeza kiwango cha fedha pekee, kwa maana hiyo serikali inatakiwa kutumia benki kama NMB ambayo imefika katika kila wilaya ili wanafunzi waweze kuchukulia fedha zao huko na sio kuja hapa Dar es Salaam.

  Naye Dk. Adolf Mkenda kutoka UDSM, alisema serikali imedai kuwa uwiano kati ya mwalimu na mwanafunzi umeongezeka ambapo sasa mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 46 badala ya 60 na kuendelea.

  Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo cha Habari na Ushauri kutoka Taasisi ya Hakielimu, Nyanda Shuli, alisema Serikali inapaswa kuhakikisha mpango wa maendeleo ya awamu ya tatu kuhakikisha zinawafikia walengwa ili kuboresha sekta ya elimu nchini.

  Habari hii imeandikwa na Gabriel Mushi, Grace Suresh na Joyce Ng’hyama, Dar es Salaam.
   
 2. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ninapata shida kuamini kuwa waheshimiwa Wabunge wanaounga mkono bajeti hii hawana huruma na watoto wa Watanzania. Hii ndiyo Tz bwana.
   
 3. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Shukuru alilengwa na makopo mwaka jana kwenye mgomo wa wanafunzi pale (main campus) , kitendo kilicho sababisha mvua ya mabomu. Kwanini asingepigwa hata jiwe ili ajifunze maana utadhani haelewi huyu jamaa! Hana hata sentensi moja ambayo ni faraja kwa ukuaji wa elimu hapa TZ. Uwezo wake upo under average.
   
 4. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
 5. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wenzetu Wakenya wanasema haya juu ya elimu yao!
   
 6. d

  dada jane JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina hamu kabisaa na elimu itolewayo Tanzania. Wakubwa hawana uchungu nayo hata kidogo.
   
Loading...