Wadau wa utalii mna mtazamo gani kuhusu uamuzi mpya ukusanyaji wa mapato yanayotokana na utalii?

Nakubaliana na wewe kabisa chief, hasa kwenye fact kwamba hii sector yetu imebase kwenye kuuza huduma kuliko product, hili sio jambo la kufanya "trial and error" experience mbaya kwa mgeni ina effects kubwa sana kwenye industry nzima na tusisahau habari mbaya huenea haraka zaidi, wote tunakubali kuwa upigaji ulikithiri sana kwenye hizi taasisi lakini swala la kucentralize mapato na kuwanyima kujiendesha sidhani kama chaguo sahihi, ukiniuliza ni jambo gani lilipaswa kufanyika ningeshauri uongozi na bodi zote za juu katika taasisi hizi zingefumuliwa ili tuanze upya.
Ngoja tuangalie huenda serikali imejifunza kutokana na makosa katika maamuzi waliyofanya ya dizaini hii mf. kama katika korosho. Hivyo wakawa na solutions za issue zinazoweza kujitokeza katika operations za utalii.
 
Back
Top Bottom