Wadau wa Usafirishaji waitaka Tanroads kurekebisha mizani zake

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wadau wa usafirishaji kutoka mikoa ya Manyara,Arusha na Kilimanjaro wameomba Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuangalia baadhi ya mizani zinazotoa majibu tofauti juu ya ongezeko la mizigo na kuleta mkanganyiko kati ya maderava na wamiliki wa malori.

Aidha Sheria ya Udhibiti Uzito wa magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 ,imeanza kutumika Tanzania na kusisitiza wadau wa usafirishaji kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za miundombinu ya barabara

Akifungua mafunzo ya siku moja ya utoaji elimu dhidi ya sheria hiyo leo Jijini Arusha,Amani Lyimo ambaye ni Mhandisi wa Barabara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, alisisitiza kuwa sheria hiyo ni muhimu kuzingatiwa kwani serikali inatumia gharama kubwa kujenga na kutengeneza miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja

Alisema endapo wamiliki wa malori,madereva na wadau kutoka Tanroads wataielewa vema sheria hiyo malalamiko mengi yatapungua ikiwemo uzito kuwa tofauti katika mizani mbalimbali

"Lazima sheria hii muielewe kwani kwa Tanzania imeanza kutumika Machi mwaka huu hivyo ni lazima mjue sheria na kanuni zake kwani kunatozo zinazokusanywa kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara"

Naye Kaimu Meneja wa Shughuli za Mizani kutoka Tanroads, Mhandisi,Japhet Kivuyo alisisitiza kuwa uzito wa mizigo unaweza kuongezeka sababu ya mizigo kucheza barabarani au magari hayo kuongezwa mizigo kusisitiza hivi sasa Tanroads imepunguza malalamiko ya madereva kwa kuweka mizani maeneo mbalimbali kwalengo la kupunguza misongamano ya magari katika mizani

Alisisitiza maderava kuacha tabia ya kuongeza mizigo kwenye malori au mabasi kwakuwasimamisha abiria au kuwafaulisha kwalengo la kukwepa kodi

Nao wadau wa usafirishaji akiwemo Zainab Mnjenja ambaye ni Mwenyekiti wa Wasafirishaji wa Malori aliiomba serikali kuangalia baadhi ya mizani iliyopo Iringa eneo la Wenda kwani ni mzani unaoongoza kwa malalamiko kati ya madereva na wamiliki wa malori sanjari na faini ya GVN ambayo inatokana na mizigo kuzidi ikiwemo baadhi ya mizani uzito kutofautiana na kuleta sintofahamu kwa maderava na wamiliki wa malori hayo ya usafirishaji.

Mmoja wa wamiliki wa Vyombo vya usafirishaji jijini Arusha, Benedict Mbereselo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya magari ya Kimotco,alipendekeza Serikali iondoe utaratibu wa kupima mabasi ya abilia kwenye mizani kama ambavyo nchi za Kenya na Uganda zinafanya.

Mberesero alisema kuwa sheria hiyo ya Afrika mashariki inatumika kwa Nchi ya Tanzania pekee na hivyo inawaumiza wao kama wadau wa usafiri Kwa sababu abilia wao wanapowasafirisha hawapimwi uzito ila mabasi yao hulazimika kupima uzito kwenye mizani na kutozwa faini Kwa fedha za kigeni

Naye Mkurugenzi wa Mabasi ya Mghamba alilalamikia hatua ya kulipishwa faini Kwa Dola za kimarekani pale basi linapokuwa limezidisha uzito katika mizani jambo ambalo linawaumiza.

Wakati huo huo, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe alisisitiza kuwa serikali imeongeza mzani wa upimaji magari eneo la Namanga Wilayani Longido na Desemba mwaka huu mzani huo utakuwa umekamilika na kuanza kutoa huduma kwa lengo la kuondoa misongamano wa magari katika mpaka wa Namanga .

Ends...

IMG_20211115_102618_883.jpg
IMG_20211115_103606_340.jpg
IMG_20211115_102930_500.jpg
 
Back
Top Bottom