Wadau wa umeme wakataa ombi la TANESCO


comrade igwe

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Messages
7,329
Likes
3,819
Points
280
comrade igwe

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2015
7,329 3,819 280
Kwa mara nyingine wadau na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kama walivyokuwa wadau wa Dodoma, Mwanza na Arusha wameligomea Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kupandisha bei ya umeme huku wakisema sababu zilizowasilishwa na shirika hilo hazina mashiko ya kutosha kushawishi bei kupanda.

Hayo yamejiri jana jijini Dar es Salaam wakati wadau na wananchi wa mkoa huo waliojitokeza kutoa maoni yao kwenye mkutano wa taftishi ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ambao ndio wahusika kwa suala hilo.Wakitoa maoni yao jana mbele ya Ewura na Tanesco, wadau hao walisema pamoja na shirika hilo kuwasilisha sababu za wao kupendekeza kupandisha bei ya umeme, lakini hazina mashiko ya kutosha kuidhinisha maombi yao.

Kwa upande wao Baraza la Ushauri la Serikali (EWURAGCC), lilisema limefanya uchambuzi wa maombi hayo na kubaini kuwa ni kweli uendeshaji wa shirika hilo una gharama kubwa kuliko fedha zinazopatikana.

Lakini sababu hiyo pamoja na nyingine zilizoainishwa na shirika hilo, hazitoshelezi kushawishi wananchi kukubali kupanda kwa bei ya umeme.

“Tumepitia sababu za Tanesco kuomba kupandisha bei ya umeme, ni kweli tumeona moja ya sababu ni kuwa shirika linaendeshwa kwa gharama kubwa kuliko fedha zinazopatikana, ila pamoja na sababu nyingine, bado hazitoshi kushawishi wananchi kukubali bei kupanda,” alisema Kaimu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Amani Mafuru.
 

Forum statistics

Threads 1,273,323
Members 490,351
Posts 30,478,040