Wadau wa Tanzanite waipongeza Serikali kufuta leseni za raia wa nje

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1550758395179.png


WALIOKUWA wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite na baadaye kuporwa mgodi wao katika mazingira tatanishi, wameipongeza serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwafutia leseni ya uchimbaji raia wa Kenya, ambao walikuwa wakifanya kazi hiyo Mirerani.

“Ni sahihi kabisa, serikali imefanya kazi kubwa (serikali hii ya Magufuli). Tumeteseka na hao raia wa nje robo karne sasa, tumehangaika sana na huyu mtu raia wa Kenya aliyepora mgodi wetu mwaka 1995.

“Anapaswa kufukuzwa nchini sasa, lakini kabla ya hatua hiyo uchunguzi dhidi yake ufanyike kwa kina ili kubaini ufisadi alioufanya katika uchimbaji wa tanzanite kwa muda wote huo,” alisema Omari Said Bikubi ambaye kwa sasa ni kipofu. Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii mjini Dodoma, Waziri wa Madini, Dotto Biteko, alitangaza kuzifutia leseni kadhaa zikiwamo za raia wa Kenya ambazo ni zenye namba PML003227/NZ, PML003387/NZ.

Aidha, alisema maombi yake ya namba PML12823/NZ, PML13036/NZ, PML23159/NZ, PML25398/NZ, PML25786/NZ na PML25789/NZ yapo katika hatua mbalimbali ya kupatiwa leseni kinyume cha sheria. Waziri ameiagiza Tume ya Madini nchini kuwachukulia hatua Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 8(2) cha Sheria ya Madini, kinakataza leseni ndogo za uchimbaji kutolewa kwa wageni.

Mapema Bikubi na mwenzake Thadei Joseph Mtingange, wakizungumza jijini hapa jana, walisema walikuwa wanamiliki mgodi namba 145 na mwenzao Abubakar Saleh Mwamba, lakini katika mazingira yasiyoeleweka mgogoro ulizuka kati yao na Anthony Ngoo ambaye ni raia wa Kenya kuhusu umiliki wa mgodi huo. Bikubu alisema Ofisi ya Madini Kanda ya Arusha, kupitia barua yake ya Machi 21, 1995, kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usuluhishi, Kitalu D, Mirerani, iliafiki uamuzi uliofikiwa na kamati hiyo kuwa Mfinange aendelee na uchimbaji katika mgodi huo.

“Ndugu Anthony Ngoo ambaye ameelezwa kuwa alikuwa mfadhili wa Mfinange hakustahili kulipia mgodi huo kama alivyofanya,” ilisema sehemu ya barua hiyo. Aidha, ofisi hiyo iliandika barua nyingine, Juni 6, 1995 kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usuluhishi, Kitalu D, Mirerani, ikimtaja Mfinange kuwa ameshalipia mgodi huo na ofisi ilikuwa inaandaa hati kwa ajili yao ambayo wangeipata baada ya muda mfupi. Aidha, barua hiyo iliitaka kamati ya ulinzi na usuluhishi kuhakikisha watu wote waliopo katika shimo hilo wanaondoka ili Mfinange na wenzake waweze kuanza kazi hapo bila bughudha alisema Bikubi. Aliyekuwa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja

Alisema Kenya na India ziliipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia tanzanite ambayo inapatikana duniani kote eneo la Mirerani pekee nchini. Alitoa mfano wa mwaka 2013, ambapo Kenya pekee ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya dola za Marekani milioni 100 dhidi ya dola za Marekani milioni 38 zilizouzwa na Tanzania, wakati, India iliuza tanzanite yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 300.
 
Hawa wadosi/wahindi /wako wanafanya biashara hapa mjini arusha kama chambo tu maeneo ya uhuru road niwaizi wa madini ya tanzanite ukipita madukani kwao nibiashara za kawaida sana wanafanya hata wazawa wanaweza kufanya ila hiyo biashara siyo anayotegemea kupanga manyumba ya msajili tanzanite ndiyo biashara yao kubwa na hili lisiwe kwa wakenya tu hata wahindi wanatakiwa kuadabishwa ni wezi wa rasilimali za taifa letu,hawana lolote kwa taifa letu inafika mahali hata ardhi yetu hawa wahindi wanachulia mikopo wakwenda kufanyia biashara nchi za magharibi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wadosi/wahindi /wako wanafanya biashara hapa mjini arusha kama chambo tu maeneo ya uhuru road niwaizi wa madini ya tanzanite ukipita madukani kwao nibiashara za kawaida sana wanafanya hata wazawa wanaweza kufanya ila hiyo biashara siyo anayotegemea kupanga manyumba ya msajili tanzanite ndiyo biashara yao kubwa na hili lisiwe kwa wakenya tu hata wahindi wanatakiwa kuadabishwa ni wezi wa rasilimali za taifa letu,hawana lolote kwa taifa letu inafika mahali hata ardhi yetu hawa wahindi wanachulia mikopo wakwenda kufanyia biashara nchi za magharibi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wahindi ni wanunuzi: kosa lao ni nini!?
 
Back
Top Bottom