Wadau wa Sekta Binafsi kukutana na Rais Magufuli ukumbi wa JNICC

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
Wadau wa Sekta binafsi nchini Tanzania wanakutana na Mh Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. leo katika ukumbi wa JNICC kwa nia ya kumpongeza Kwa mafanikio ndani ya miaka mitano
 
Hivi kwa akili yako unadhani kuna ikulu ya huyo jamaa yenu ambaye ameshaadhibiwa kwa utovu wa nidhamu?? Jaama yenu kashapoteza sifa za kuwa kiongozi wa umaa. Hakuna kiongozi wa uma mwongo mwongo . hata jamaa yenu analijua hilo.
Wewe wasema
 
Jiwe hajielewi aisee. Yaani kama Kuna kundi lililoumizwa na utawala huu ni wafanyabiashara. Kwa kuwa kalazimisha wamelazimika kukutana naye tu lkn haimuongezei mileage yoyote kisiasa.

Magufuli akubali tu kuwa alilikoroga Basi alinywe tu.
Sikiliza hapa jinsi alivyokuwa anasema mbovu siku za nyuma.
 
Mkuu JINGA, hata JPM akutane na nani, awamu hii hachomoki, lazima arudi chato kama raia na raisi mstaafu.
 
Wadau wa Sekta binafsi nchini Tanzania wanakutana na Mh Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. leo katika ukumbi wa JNICC kwa nia ya kumpongeza Kwa mafanikio ndani ya miaka mitano
Waache unafiki umeme kila siku unakatwa watu hatufanyi kazi, kazi nyingi zimechukuliwa na serikali kwa kifupi ameua sekta binafsi huu unafiki huu ndio unamfanya asiweze kujirekebisha
 
Hio ni sherehe ya kumuaga, wamfundishe kujiajiri ili trh 28 mkataba wake utakapoisha rasmi asipate tabu ya maisha ya mtaani.
 
Hivi kwa akili yako unadhani kuna ikulu ya huyo jamaa yenu ambaye ameshaadhibiwa kwa utovu wa nidhamu?? Jaama yenu kashapoteza sifa za kuwa kiongozi wa umaa. Hakuna kiongozi wa uma mwongo mwongo . hata jamaa yenu analijua hilo.
Kweli kabisa kiongozi muongo kama alietudanganya kitambulisho cha machinga unaweza chukulia mkopo hatufai na hafai kuwa kiongozi wa uma.
 
Hata akutane na Malaika Ikulu, hakuna kitachobadilika.Hatufai na hatumtaki.

Anataka kujisafisha mbele ya wafanyabiashara ili asionekane kawaumiza.
 
Sisi bosi wetu katuambia hicha kikao kaudhuria tuu basi hana namna ila katuomba Heads of Department kuwahamasisha staff walio chini yetu kuchagua upande wa Haki , Uhuru na Maendeleo ya watu , ametujuza swala la Kikokotoo kwani hata yeye halimfurahishi anavyoona kuwa anatuchania 10% ya NSSF zetu ila anajua tutachukua miaka kufaidi michango yetu

Vile vile hapendezewi ya majina waliyopewa na Polepole Bashiru, Magu na yule Waziri wa mambo ya nje kuwa wao ni mabeberu kisa rangi yake siyo sawa ya ya kwetu

Amechukizwa sana na swala la TRA kubambikia kodi kwa nguvu na kushikilia accounti zetu za bank kwa kodi za uongo na za kulazimisha

Alichukizwa sana na kitendo cha kusema matajiri na wafanya biashara wataishi kama mashetani kwani huo ni mpango mkakati wa kuwafukuza na kupoteza ajira zetu

Kwa hiyo basi wafanya kazi wote wapatao 991 tumaitikia wito wa bosi wetu na tutachagua upande wa haki Uhuru na maendeleo yetu
 
Wadau wa Sekta binafsi nchini Tanzania wanakutana na Mh Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. leo katika ukumbi wa JNICC kwa nia ya kumpongeza Kwa mafanikio ndani ya miaka mitano
Hawa wanatafuta fursa ya kuzitumia pesa zilizoko ndani ya uwezo wao wa matumizi 'they are opportunity seekers'
 
Back
Top Bottom