Wadau Wa Muzik Wa Zamani Tukutane Hapa.

Gooodwin

Member
Sep 22, 2016
77
66
Kuna bendi ikikuwa inaitwa washirika tanzania stars, Watunjatanjata wameimba nyimbo kali kama vile Julie,penzi laulaghai naomba kujuzwa ile sauti kama ya kike ni ya nani siku zote mimi nilikuwa najua ni ya Kida Waziri.
 
Huyo ni Marehemu Eddy Shegy kabla ya Washirika alikuwa Vijana jazz na sauti yake unaweza kuisikia vizuri kwenye nyimbo kama Ogopa tapeli na Wivu.
 
Huyo ni Marehemu Eddy Shegy kabla ya Washirika alikuwa Vijana jazz na sauti yake unaweza kuisikia vizuri kwenye nyimbo kama Ogopa tapeli na Wivu.
Naam kwanza aelewe kasema washirika sasa kida waziri anaingiaje hapo? Kuhusu sheggy huyo mtu basi tu mimi nilianza kumkubali penye milima ya kwetu akiwa na super rainbow kisha kuna kibao kingine cha kuitwa chaurembo hapo tayari yupo vijana maana alianza yeye kuimba verse ya kwanza kisha akaingia mzee mzima maneti "chiriku"watu ndio tukajua amekwenda vijana.
Chaurembo
Fanya yote lakini ukumbuke maisha ni mlima
Kuna kupanda na kushuka yeyeeye
Kwani kuteleza sio kuanguka
Chaurembo mamaeee
 
Wewe unakumbuka nini kuhusu muziki na wanamuziki wa zamani.Jee unajua kisa chochote kuhusu wimbo fulani au mwanamuziki fulani?Au nini kilikutokea wakati ulipokuwa katika kufurahia muziki huo?Tuwe huru kujadili muziki kuanzia hapa nyumbani,Zaire,Ulaya mpaka kule Marekani.

Kwa upande wangu niliyatumia maneno katika wimbo;Sarah nyota ya uzuri ulioimbwa na Jerry Nashon akiwa na Bima Lee,nikajipatia mke!Nikijifanya hizo verse ni zangu.Baadhi ya maneno katika wimbo huo ni haya;
Nilipokuona kwa mara ya kwanza,nilishikwa na butwaa ,nilichanganyikiwa eeeh.
Sijui niimbe nyimbo gani ili ujue nakupenda.Hiii Sarah nyota ya uzuri.Natamka nakupenda sana.
Kwani sina mtu mwingine ambaye roho yangu imeridhika nayee.

Karibuni
 
Naukumbuka wimbo mmoja tulikuwa tunaimba zamani sana, mwaka 1208 kabla ya kristo, kutokana na teknolojia ya wakati huo haukurekodiwa kokote. Kwa hiyo hamna aujuaye
 
Naukumbuka ule wimbo wa Mbaraka Mwinshehe wa jogoo la shamba haliwiki mjini........

Ile ni true story ambapo 'mshamba' mmoja toka Mikese alipoambulia kichapo kutoka kwa mdogo wake Mbaraka baada ya huyo jamaa kujifanya mbabe kwenye show mojawapo ya bendi ya Super Volcano pale mji kasoro bahari........
 
Oooh jamani binadamu hatosheki
Hata ukimpa nini (Nyerere )hata ridhika
Kimbembe kilikuwa hapo badala ya kusema milele sisi tuliimba Nyerere mzee makasy hapo enzi hizoooo siku hizi anaimba pambio .
 
Back
Top Bottom