Wadau wa JF, ni Mkono/Mguu wa Kulia au wa Kuume? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau wa JF, ni Mkono/Mguu wa Kulia au wa Kuume?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kichankuli, Dec 18, 2008.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2008
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Watanzania tunaaminika kuwa ndiyo wenye asili ya Lugha ya Kiswahili. Lakini kuna maneno mengi ambayo tumekuwa tukiyatumia isivyostahili. Mathalan, ni lipi jina sahihi la mkono ambao wengi wetu huwa tunautumia sana kama kiongozi wa shughuli zinazofanywa na miili yetu, je ni mkono wa kuume au wa kulia?.

  Ningependa nipate maoni yenu wadau wa JF kabla na mimi sijatoa yakwangu ninayoyafikiria. Uwanja ni wenu
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kichankuli... Ni che mosi?

  Majibu yote ni sahihi... Kwani Kandili na taa si kitu kilekile?
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Yanaashiria maana moja lakini matumizi yake hutegemea sana muktaza (context). Kwa mfano nadhani si sahihi kusema 'mkono wa kuume'; sahihi ni 'mkono wa kulia'. Vivyo hivyo si sahihi kusema 'upande wa kulia'; bali 'upande wa kuume'.
   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2008
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Fikra zangu zinanituma kwamba usahihi ni mkono/mguu kuitwa wa kuume. Aidha fikra zangu zinanieleza kwamba matumizi yaliyozoeleka sana ya kuuita mkono wa kulia yanatokana na desturi za Kiafrika kwamba mkono wa kuume ndiyo haswa makhsusi kwaajili ya kuchukua, kusafirisha na kukitia mdomoni chakula. hebu angalia sentensi hizi:
  1: Chumba cha kulia chakula
  2: Meza ya kulia chakula
  3: Kijiko cha kulia Ubwabwa
  4: Mboga za kulia chakula cha jioni
  5: Sahani ya kulia makande

  Sasa mkono wa kulia chakula ni upi? kwa waafrika ndo mkono wa kiume; kwa wazungu ambao wanatumia mikono yote, wakati mwingine, huku uma na huku kisu sijui jibu litakuwa lipo
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kama alivyosema mkuu SMU hapo juu yote ni sawa lakini matumizi yake hutegemea zaidi muktadha,ie jinsi(lengo) unavyotaka kulitumia neno husika(angalia mfano wa SMU hapo juu)
   
 6. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #6
  Dec 18, 2008
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  upande wa kuume nimesikia leo hii (MALI MPYA) mkono wa kuume ndio kawaida.
   
Loading...