Wadau wa elimu: Hivi itanichukua muda gani kurejesha deni HESLB?

Kiwangwa Son

Senior Member
Nov 29, 2018
178
115
Habari ya muda huu wakuu,

Kama kichwa kinavyojieleza mimi ni mwanafunzi nipo chuo fulani hapa nchini kwa sasa nipo mwaka wa nne nasomea ufamasia.

Kutokana nipo chuo cha private na mkopo nilibahatika kupata asilimia mia moja(100%)

Hivyo nimepiga calculations nimeona kwa miaka miaka minne niliyosoma hapa chuoni nitakuwa nadaiwa sio chini ya millioni ishirini na tatu (23).

Lengo la kuja kwenu nilikua nahitaji wajuzi na wahanga wengine mjaribu kutoa uzoefu wenu .

Je, kwa madeni makubwa kama haya marejesho yake huwa yanadumu kwa muda gani?

Je, kama najiajiri au naajiriwa miaka kumi(10) itatosha kumaliza deni na kuendelea na maisha yangu binafsi?

Ahsante karibuni.
 
Me engineering naitazama Tsh million 16 roughly, ukifikilia deni unalodaiwa na ugumu wa masomo unaokutana nao akili lazima ikuwake moto.
 
Hilo deni ni kama unafanya scientific research hua haliishi kila mwaka litapanda na kushuka... Achana nalo litakuumiza kichwa tu fanya mambo mengine
 
Back
Top Bottom