Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,005
- 1,583
WADAU wa sekta za biashara na usafirishaji wameitaka serikali kutoipa kampuni ya TICTS mkataba mpya wa kuendesha eneo la kontena la bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa limeshindwa kufikia lengo la kuongeza wingi wa mzigo kwa asilimia 37 kwa mwaka na kushindwa kuwekeza kwenye miundombinu ya bandari.
Kusuasua kwa Kampuni hiyo kumeongeza gharama ya kuingiza mizigo nchini na kulikosesha Taifa mapato kutokana na wafanyabiashara wa nchi jirani kuamua kuikwepa bandari ya Dar es Salaam na kukimbilia bandari za Kenya, Afrika Kusini na Namibia zenye ufanisi zaidi.
Chama wa Mawakala wa Forodha (TAFFA) kimelalamika mara kadhaa kuhusu TICTS kuwa na ufanisi mdogo na kusababisha ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Wabia wa TICTS ni pamoja na waziri wa zamani Nazir Karamagi na mfanyabiashara maarufu Yogesh Manek, wakishirikiana na mwekezaji wa nje, kampuni ya Hutchinson Ports ya Hong Kong.
Taarifa kutoka bandarini zinaonesha kuwa TICTS walipewa nyongeza ya mkataba wa miaka mitano mwaka 2017 baada ya kushindwa kuleta ufanisi tangu wapewe kuendesha eneo la kontena la bandari ya Dar es Salaam zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Chanzo: Nipashe