Wadau ukienda choo cha ugenini kabla hujajisaidia hakikisha kama kuna maji ndio uchuchumae

kuna fala mmoja nilikua naishi nae nyumba moja ya kupanga hivyo tuli share choo, jamaa ana umri si chini ya miaka 40 na alihamishiwa kikazi huo mkoa akitokea mara huko
bwana yule alikua akiingia chooni haflash yani anaacha mchongo unaelea tu,ukiingia ni kinyaa cha hatari
😂😂😂 Mchongo😂😂
 
Pole Sana kwa yaliyokusibu ,

Kiuhalisia watu tupo tofauti , inavyokua siku yeyote ukipata mgeni yeyote kaja kwako na mgeni kakupa alert anataka kwenda chooni lazima ww mwenyeji uhakikishe Kama maji yapo, Kama hakuna maji muwekee kisha ndio umruhusu kwenda huko chooni .

OK sawa nimejifunza pia kutoka kwako ,,tahadhar muhimu
Nakubaliana na wewe mkuu

Lazima mwenyeji ahakikishe kila kitu kipo sawa kabla mgeni hajaenda washroom
 
Pole sana. siku ingine uwe unaweka kupande cha toilet paper mfukoni kama vile unavyoweka henka. Ungejifuta vizuri tu na kuvaa na kuenda kuomba maji. Halafu hakuna sabuni unajifuta na maji. saa ingine harufu haitoki mkononi hili unalijua? Huwa mnafanyaje juu ya hili? Maana inategemea chakula ulichokula.
 
Wadau naandika nikiwa katika hali ya huzuni mode. Kuna binti mmoja ambaye kiuhalisia namkubali sana, ni mzuri, msomi na mtu wa dini sana.

Last week alinialika kwao nikamsalimie mama yake coz kidogo alikuwa na mgogoro kiafya. Nami kwa kuwa nataka palilia uhusiano nikaona nisikose kufanya tembezi hilo la mshikamano.

Ghafla tumboni kulitokea hali ya kutokuwa na maelewano, ubishani ukawa mkubwa nikalazimika kwenda msalani kutafuta usuluhishi, nliharisha sana.

Nlipomaliza nikataka sasa kujiswafi, ndio kugundua maji hamna. Hayatoki hata kutaka kuflash ikawa ngumu pia. Hamna maji, jasho likaanza nitoka.

Nilikaa kama dakika 20 nikitafakari na kufanya maombi maji yatoke na mara nikasikia mtu anazungusha kitasa, nikakohoa kidogo kuonesha kuna mtu.

Hali ilipozidi nikakumbuka kuwa choo kipo mwisho kabisa wa korido na sebuleni kunaonekana, nikainuka huku nmeshikilia suruali kwenda chungulia kama yule dada anaweza niona ili nimwite. Nimesubiri sana nikichungulia mara nikamwona ameinuka hapo nikafanya ishara kumwita.

Daaah...maskini, wakati namkonyeza na kaka yake baunsa akawa anaingia. Akaona nipo chooni nachungulia huku nafanya ishara ya kumwita dada yake. Jamaa alinitizama kwa mshangao sana. Yaani nikaona kabisa kama amekuwa mwekundu kwa ghadhabu.

Najua alihisi namwita dada yake nikamkamulie chooni. Daah nami ule mshtuko nikajikuta namwamkia but hakuwa wa kuamkiwa kabisa na mimi nikaropoka "chooni hamna maji" jamaa akaingia room kwake.

Daaah...mimi hali yangu mbaya maana harufu imekuja hadi koridoni, ikabidi tu nimwite bintI akaja nikamweleza. Akaenda fungulia tanki maji yakaja nikafanya usafi.

NIlipoteza amani kabisa, ni jambo ambalo limenifedhehesha sana. Sielewi waliongea nini after my departure maana ile ilikuwa ni dhahma kwangu.

Wadau ukienda choo cha ugenini kabla hujajisaidia hakikisha kama kuna maji, hakikisha sana ndio uchuchumae ushushe mzigo.
Noorah aka Baba styles alishazungumzia kwenye vijimambo so hakuna jipya.....ila asante kurudia story.
 
Ndio maana ikitokea ukanisachi mfukoni, mbali na fedha na simu, lazima utakutana na kipande kirefu cha toilet paper.

Yalishawahi kunikuta ndio maana siachi kutembea na kipande cha karatasi hizo za chooni.
 
Wadau naandika nikiwa katika hali ya huzuni.

Kuna binti mmoja ambaye kiuhalisia namkubali sana, ni mzuri, msomi na mtu wa dini sana. Last week alinialika kwao nikamsalimie Mama yake kwasababu kidogo alikuwa na mgogoro kiafya. Nami kwa kuwa nataka palilia uhusiano nikaona nisikose kufanya tembezi hilo la mshikamano.

Ghafla tumboni kulitokea hali ya kutokuwa na maelewano, ubishani ukawa mkubwa nikalazimika kwenda msalani kutafuta usuluhishi, niliharisha sana.

Nlipomaliza nikataka sasa kujiswafi, ndio kugundua maji hamna. Hayatoki hata kutaka kuflash ikawa ngumu pia. Hamna maji, jasho likaanza nitoka.

Nilikaa kama dakika 20 nikitafakari na kufanya maombi maji yatoke na mara nikasikia mtu anazungusha kitasa, nikakohoa kidogo kuonesha kuna mtu.

Hali ilipozidi nikakumbuka kuwa choo kipo mwisho kabisa wa korido na sebuleni kunaonekana, nikainuka huku nimeshikilia suruali kwenda chungulia kama yule Dada anaweza niona ili nimwite. Nimesubiri sana nikichungulia mara nikamwona ameinuka hapo nikafanya ishara kumwita.

Dah! maskini, wakati namkonyeza na Kaka yake baunsa akawa anaingia. Akaona nipo chooni nachungulia huku nafanya ishara ya kumwita Dada yake. Jamaa alinitizama kwa mshangao sana. Yaani nikaona kabisa kama amekuwa mwekundu kwa ghadhabu.

Najua alihisi namwita dada yake nikamkamulie chooni. Daah nami ule mshtuko nikajikuta namwamkia but hakuwa wa kuamkiwa kabisa na Mimi nikaropoka "Chooni Hakuna Maji" jamaa akaingia room kwake.

Mimi hali yangu mbaya maana harufu imekuja hadi koridoni, ikabidi tu nimwite bintI akaja nikamweleza. Akaenda fungulia tanki maji yakaja nikafanya usafi.

Nilipoteza amani kabisa, ni jambo ambalo limenifedhehesha sana. Sielewi waliongea nini after my departure maana ile ilikuwa ni dhahama kwangu.

Wadau ukienda choo cha ugenini kabla hujajisaidia hakikisha kama kuna maji, hakikisha sana ndio uchuchumae ushushe mzigo.
Pole sana mkuu, kilichobaki sasa ukawa unatafuta namna ya kuwathibitishia ni kwa nini ulimwita binti wao.

Sent from my cupboard using mug
 
Nacho hicho choo kilikuwa na cha uswahilini ndani ndani sana!

Choo cha kistaarabu kitakosaje 'rola' ya toilet paper ambayo ndiyo ingelikuwa huduma ya kwanza na msaada wako wa kuanzia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom