Wadau: Tanzania Muungeni mkono Mwanamuziki JettyMan

superwarkills

Senior Member
Aug 18, 2014
136
83
Anaitwa Samson Noha...(Maarufu kama Jettyman),Licha ya changamoto ya kiafya anayopitia zaidi ya miaka 6 sasa lakini amekuwa akifanya muziki wake akiwa kitandani,na zaidi sasa amekuwa ni producer mzuri kabisa.

Kwa wale wanaokumbuka ule wimbo wenye introduction "kama naikumbuka hivi inasema.

OgopaDjs wanafanya Unadata (unadata) halaah baby.

and zed hala baby.

Tunaweza kusema Jetman ndiye mwanamuziki aliyeuwakilisha muziki wa ndancehall katika matamasha mbalimbali jijini mwanza baada ya kutoka kufanya kazi yake nchini kenya chini ya studio za OgopaDJz, vilevile nje ya muziki Jettyman ni fundi na mbunifu mzuri sana wa mavazi kabla ya kupata changamoto ya kiafya,
Jettyman Mwanamuziki na mshirika mkubwa katika familia ya Dolphine pose iliyokuwa maeneo ya Pasiansi Mwanza na
Wanamuziki wengine Kama Jontwa John, Rweymam, Phantom Ranks, Soo face, Bundo, Mwanadada Lady Luu(Mungu amlaze mahali pema) Longman, Maximum 1&2, Godman na wengineo.

Kinachotia moyo ni kuwa licha ya Jetman kuwa kitandani kwa miaka kadhaa toka apate changamoto hiyo bado hajakata tamaa ameendelea kupenda na kujikita katika muziki na zaidi kwa sasa anazalisha vizuri tu muziki.

Kwa wanaokumbuka katika kampeni ya #Riddim ya mfalme, ni mdundo(beat) uliotengenezwa na jettyman, mdundo ambao Waziri wa Habari na utamaduni wa sasa Mh. Nape Nnauye aliuimbia katika kampeni ya #AMKANAJETMAN iliyoendeshwa na kituo kimoja cha redio.

Habari nzuri ni hii..

Kwa Sasa Jettyman nilipata taarifa kuwa anaandaa eneo lake la kufanyia kazi(Studio) ambalo lipo kabisa katika hatua za mwisho(finishing) ili aweze kuhamishia kazi zake karibu wadau wake tofauti na sehemu alipo sasa.

Ombi langu kwa wadau na wapenzi wa muziki Mwanza, na East Afrika kwa ujumla ni ikiwapendeza kumuunga mkono mwanamuziki huyu ili aweze kumalizia mkia huo kidogo(ene) japo ng'ombe si mkubwa sana (kama Mlango, top, furniture n. k) kwa kadri utakavyoguswa.

Mwenyezi Mungu awaguse kwa kadri ya hali zetu kuleta tabasamu kwa wengine.

0763 484 006 Jina Samson Noha

0621 333 277 Samson Noha

Mbarikiwe

Polish_20220303_132759575.jpg
 
Anaitwa Samson Noha...(Maarufu kama Jettyman), Licha ya changamoto ya kiafya anayopitia lakini amekuwa akifanya muziki wake akiwa kitandani,na zaidi sasa amekuwa ni producer mzuri kabisa.

Kwa wale wanaokumbuka ule wimbo wenye introduction "kama naikumbuka hivi inasema.

OgopaDjs wanafanya Unadata (unadata) halaah baby.

and zed hala baby.

Tunaweza kusema Jetman ndiye mwanamuziki aliyeuwakilisha muziki wa ndancehall katika matamasha mbalimbali jijini mwanza,nje ya muziki Jettyman ni fundi na mbunifu mzuri sana wa mavazi kabla ya kupata changamoto ya kiafya, Jettyman Mwanamuziki na mshirika mkubwa katika familia ya Dolphine pose iliyokuwa maeneo ya Pasiansi Mwanza na
Wanamuziki wengine Kama Jontwa John, Rweymam, Phantom Ranks, Soo face, Mwanadada Lady Luu(Mungu amlaze mahali pema) Longman, Maximum 1&2 na wengineo.

Kinachotia moyo ni kuwa licha ya Jetman kuwa kitandani kwa miaka kadhaa toka changamoto hiyo bado hajakata tamaa ameendelea kupenda na kujikita katika muziki na zaidi anazalisha vizuri tu muziki.
Kwa wanaokumbuka katika kampeni ya #Riddim ya mfalme, ni mdundo(beat) uliotengenezwa na jettyman, mdundo ambao Waziri wa Habari na utamaduni wa sasa Mh. Nape Nnauye aliuimbia katika kampeni ya #AMKANAJETMAN iliyoendeshwa na kituo kimoja cha redio.

Habari nzuri ni hii..

Kwa Sasa Jettyman nilipata taarifa kuwa anaandaa eneo lake la kufanyia kazi ambalo lipo kabisa katika hatua za mwisho(finishing) ili aweze kuhamishia kazi zake karibu wadau wake.

Ombi langu kwa wadau na wapenzi wa muziki Mwanza, na East Afrika kwa ujumla ni ikiwapendeza kumuunga mkono mwanamuziki huyu ili aweze kumalizia mkia huo kidogo japo ng'ombe si mkubwa sana (eneo)

Mwenyezi Mungu awaguse kwa kadri ya hali zetu kuleta tabasamu kwa wengine.

Instagram


Mbarikiwe​


View attachment 2140610
Jamaa kaumwa muda mrefu, kuna kipindi aliomba msaada enzi za ruge wakamchangia changia akatengeneza beat watu wakawa wanapita nalo kwa kulilipia hata fid q alipita nalo lakini sidhani kama ela ilitosha
 
Jamaa kaumwa muda mrefu, kuna kipindi aliomba msaada enzi za ruge wakamchangia changia akatengeneza beat watu wakawa wanapita nalo kwa kulilipia hata fid q alipita nalo lakini sidhani kama ela ilitosha
Sana sema jamaa bado aendeleza muziki wetu licha ya kuwa kitandani miaka mingi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom