Wadau nisaidieni mawazo.. Tigo niwafanye nini..?

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,539
9,462
Uciku wa kuamkia tarehe 3 mwezi wa 11 nilinunua muda wa maongezi kwa tigopesa wa shilingi 18,000.. Cikupata message kuonyesha kama transaction imefanyika na wala credit haikuingia.. Asubuhi nikajaribu tena kununua muda wa maongezi wa kiaci kile kile cha shs. 18,000.. Nikapata msg kwamba salio langu halitoshi.. Kuangalia salio kwenye tigo pesa nikakuta imebaki minus 18,000.. Nikawapigia tigo na baada ya kuangalia wakasema kweli wameona hela imekatwa toka kwenye akaunti tigo pesa lakini haikuingia kwenye muda wa hewani.. Wakaahidi kulitatua tatizo ndani ya masaa 24 kwa kurudishiwa salio kwenye tigo pesa..

Pamoja na bidii zote za kufuatilia kwa kupiga cimu mara kwa mara na kwenda kwenye kituo cha tigo kulalamika cijalipwa mpaka leo hela yangu..

Naomba members mnisaidie nifanye kitu gani nipate haki yangu.. Au kama kuna member ambae yuko Tigo naomba kusaidiwa mawazo cha kufanya.. Au nipate namba ya ambae anaweza kulitatua hili tatizo..
Shs. 18,000 inaweza kuwa ndogo but ni haki yangu ambayo ciko tayari ipotee..
 
nenda mahakamani ukisndikizana na waandishi wa habari watakulipa na ziada kwa kuogopa aibu
 
nenda mahakamani ukisndikizana na waandishi wa habari watakulipa na ziada kwa kuogopa aibu

Ha ha ha.. Mkuu Kibaa kuwabeba waandishi wa habari ni gharama nyingine.. Au umesahau bila ya vibahasha huwapeleki mahali wale..?
 
nenda mahakamani ukisndikizana na waandishi wa habari watakulipa na ziada kwa kuogopa aibu

Wanatumia udhaifu wa mfumo wetu wa kudai haki ya hela ndogo ndogo, wanajua uwezi kutumia muda mwingi na hela nyingi kwenda mahakamani kudai chini ya laki moja, njia ni hiyo ya waandishi wa habari kuwalipua lakini na wao wanalijua hilo, ukitoa stori kwa waandishi wa habari wataenda ku balance stori tgo wakifika huko wanarudi na bahasha, halaf stori inaishia hapo, au wakiitoa inatoka poa.
 
Pole sana, tigonwan vimechezo vibaya mi mwenyewe wamenitenda, though casenyangu ni tofauti kidogo, mi nilinunua bundle ya 30,000 yenye internet na sms 1000, hah nimeshangaa kesho yake naambiwa nimemaliza sms zote 1000! Hadi nikahesabu sms maana sikua nimefuta zikaishia 100 nikapiga nikaambiwa baada ya masaa 24, sikusaidiwa, nikapiga wapi, inaniuma big tyme. Ukipata solution/cha kuwafanya niambie tushirikiane
 
nikapiga nikaambiwa baada ya masaa 24, sikusaidiwa, nikapiga wapi, inaniuma big tyme. Ukipata solution/cha kuwafanya niambie tushirikiane

Ahsante Babe S.. Ndo zao kukuambia ndani ya masaa 24.. Wateja wengi wanalalamika kuchukuliwa hela zao japo ndogo ndogo kwa mtindo huo.. Nitakujuza pindi tu nipatapo solution.. Maana hata ku-post hapa ni katika kutafuta solution..
 
Tigo ni serikali ndani ya serikali. Haya ndiyo matokeo ya kuwa na watawala wafanyabiashara. Tunalanguliwa na kuibiwa mchana na hakuna linalofanyika kutokana na taasisi zetu zote kuwa mikononi mwa wawekezaji ambao kimsingi si wawekezaji kitu bali wachukuaji. Ningekuwa wewe ningeenda kwenye magazeti na televisheni kuwalipua. Jaribu watu wa magazeti ya udaku uone watakavyowapaka.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom