Wadau ninaomba ushauri: Binti wa Form 4 asomee nini kutoka haraka kiuchumi?

Issue Ni cheti kozi zipo ila vizuri kabla kushauri vyuo Mleta mada tuwekee pass zake hapa
 
Wapendwa wasalaam.
Binti yangu aliyemaliza Form 4 na hakufanikiwa kuendelea na vidato. Ninaomba ushauri wa kozi kama ni ufundi au chochote ambacho kitampa ajira na kipato kwa haraka. Natanguliza shukrani.
walaykum salaam, kushindwa kufanya kitu fulani vizuri ndio kujifunza...mwanao kiumri anahitaji kuelimika.ila kama wazo lako ni ajira na kipato (ingawa duniani vipato vya haraka vinamatatizo) , Ajira anaweza kujiajiri mwenyewe, kipato ni matokeo ya kujituma kwa hali ya juu. Kitu cha kufanya mwangalie anapenda kufanya shughuli gani sana? hiyo ndio ya kuifanyia kazi, na la mwisho ajifunze elimu ya ujasiliamali
 
Wapendwa wasalaam.
Binti yangu aliyemaliza Form 4 na hakufanikiwa kuendelea na vidato. Ninaomba ushauri wa kozi kama ni ufundi au chochote ambacho kitampa ajira na kipato kwa haraka. Natanguliza shukrani.
Aanze certificate aidha nursing au pharmacy
 
Kuna veta huko wanafundisha :
1- mafundi ujenzi
2- mafundi magari
3- mafundi rangi wa nyumba
4- cherehani afu ukamfungulia garment mkuu.
Yaani mtafiti kwanza anapenda kufanya nini.
Maisha huwa yamo ama yanapatikana kwa kufanya unachokipenda mkuu ila sio cha kushauriwa. Ni sawa na mapenzi oa unayempenda ila siye aliyependwa na wazazi,marafiki,ndugu zako
Mafundi ya vitendo akafanyie kwa Fundi Maiko
 
Mkuu Keisangora, nimependa hiyo foreign language. Unaweza kunisaidia chuo kinachotoa kozi hiyo?
Kuna wajerumani Fulani wana chuo kipo Arusha na dar kinaitwa GOETHE.DE mkuu wacheki.pia kwa Arusha utapata chuo hata cha Spanish Nina imani.
Kama Russian language Ukienda Tanzania-Russian Cultural centre utapata Huduma iyo.pia kama ni Danish,Norwegian&Swedish language Ukienda dar kama unaenda IST wana shule zao za Nordic countries uwaulizie. Kuna Mdada mmoja pale ni mchaga wanafundisha shuleni hapo ila yeye anakula Swedish mkuu.
Pia ninaomba sana utumie mtandao kama una interest ya kujifunza kitu. K.v YouTube wako Poa sana.Tumia bando kula knowledge na sio kupostia picha social network ukiwa unakula kuku ila siku ukila maharage hauposti.
Katika ulimwengu huu tunaoishi kila maarifa yapo wazi kazi kwako kuyachota.
Kirusi kama Uko interested nicheki nakufundisha ila gharama ni ruble 1000 kwa lisaa.

Pia kichina na kireno kinafundishwa pale udsm katika College ya CoSS kama sijakosea ni siku nimetoka Hayo maeneo mkuu

Mkuu kupost picha sijakulenga www ni jamii nzima ya kitanzania namie nikiwemo
 
Wapendwa wasalaam.
Binti yangu aliyemaliza Form 4 na hakufanikiwa kuendelea na vidato. Ninaomba ushauri wa kozi kama ni ufundi au chochote ambacho kitampa ajira na kipato kwa haraka. Natanguliza shukrani.
Kasoma mchepuo gani ?
 
Kuna wajerumani Fulani wana chuo kipo Arusha na dar kinaitwa GOETHE.DE mkuu wacheki.pia kwa Arusha utapata chuo hata cha Spanish Nina imani.
Kama Russian language Ukienda Tanzania-Russian Cultural centre utapata Huduma iyo.pia kama ni Danish,Norwegian&Swedish language Ukienda dar kama unaenda IST wana shule zao za Nordic countries uwaulizie. Kuna Mdada mmoja pale ni mchaga wanafundisha shuleni hapo ila yeye anakula Swedish mkuu.
Pia ninaomba sana utumie mtandao kama una interest ya kujifunza kitu. K.v YouTube wako Poa sana.Tumia bando kula knowledge na sio kupostia picha social network ukiwa unakula kuku ila siku ukila maharage hauposti.
Katika ulimwengu huu tunaoishi kila maarifa yapo wazi kazi kwako kuyachota.
Kirusi kama Uko interested nicheki nakufundisha ila gharama ni ruble 1000 kwa lisaa.

Pia kichina na kireno kinafundishwa pale udsm katika College ya CoSS kama sijakosea ni siku nimetoka Hayo maeneo mkuu

Mkuu kupost picha sijakulenga www ni jamii nzima ya kitanzania namie nikiwemo
Duh mkuu nashukuru sana. Ngoja nianzia CoSS Maana nimefanya nao kazi pia
 
Nawashukuru sana ingawa bado natafuta "quick win" moja ambayo akimaliza tu anatoka. Umenena vyema mkuu. Na ndiyo haswa lengo, sitaki akae ndani bila kufanya kitu. Hayo mengine ningependa yamkute akiwa kazini kwake ili hata likitokea aweze kumudu mwenyewe.
Bar attendant course
 
Back
Top Bottom