Wadau naombeni Msaada please. Nimepatwa na Janga

But huyo nyoka ndo atakuwa amekuja kwenye anga za huyu jamaa yangu. Huyu mbwa hatoki kwenye gate isipokuwa jioni anatolewa akajisaidie na asubuhi haraka anarudi. Leo hata nje ya gate imebidi apelekwe. Sasa inabid kuanzisha MSAKO WA HAYAWANI HUYU. huyu bwana mdogo anakomaa tu kuwa ni mama jirani ndo tatizo.ashawahi sema yeye hapendi mbwa. Na jana alikuja kama bundi. Nlisikia mimi sauti ya bundi but i didnt give a damn . Sasa bwana mdogo anakazia hapo hapo aiseee...

Mama wa jirani angetumia utamaduni saa hizi ingekua matanga...si umeona kamanda ameanza kuona kwa mbali? Atakaa sawa tu.
 
Ni week sasa nipo jiji la Mwanza kwa mapumziko ya mwisho wa Mwaka. Nina sehemu nimeweka kakibanda na ufugaji na mapumziko pia.

Leo nmeamka asubuhi mmoja ya Mbwa wangu kapoteza ghafla uwezo wa kuona. Mbwa wapo wawili.hawakugombana na huwa hawana tabia ya kugombana.

Hajaumia popote pale ila haoni kabisa ingawa macho yapo wazi. Jana usiku amefunguliwa alikuwa Ok kabisa. Leo asubuhi nmeamka nifanye mazoezi namwambia kuingia ndani anazunguka tu akijigonga. Nlishangaa.baadaye nimegundua haoni.

Hata nikipitisha mkono mbele yake haoni. Zaidi zaidi anaonekana kunusa.nimepata mawasiliano na daktari wa mifugo nimemweleza anasema hajui tatizo nini.

Nimekosa raha,sina amani nataka kumsaidia huyu Mbwa maana ni mbwa mwema kabisa.very friendly kwangu na hatari kwa maadui. Huyu kijana ambaye hukaa hapa anahusisha jambo hili na imani za kishirikina.mimi sielewi hayo mambo.

Naombeni msaada namsaidia vipi mbwa wangu. Na huku niliko Madaktari wa mifugo wachache maybe niende town. But daktari mmoja huyu ndo amenambia hajui tatizo ni nini.maana macho yanaonekana hayana ugonjwa wowote na hayadhurika.ameshindwa la kufanya.


huyu bwana mdogo anakomaa tu kuwa ni mama jirani ndo tatizo.ashawahi sema yeye hapendi mbwa. Na jana alikuja kama bundi. nami nlisikia mimi sauti ya bundi but i didnt give a damn . Sasa bwana mdogo anakazia hapo hapo. Nimeshapoteza mbwa kama wanne hapa toka nimeanza fuga.

Jirani mama huyu hapendi mbwa ingawa hawafiki kwake coz hapa kuna fance. Pia mbwa ashasaidia zaidi ya mara nne kumwonesha kijana Nyoka. So its possible ni nyoka. Ingawa kijana hakubali kabisa
Naaam Pdf yake ni kubwa kidogo.
 
Pia paka humtemea mate Mbwa Wakiwa kwenye kurupushani .
Yanakuwa na Blue na matongo tongo ya kuzidi
Pia ukimchunguza utakuta kwenye kope pasipo na manyoya kuna vimichirizi vya vidonda

Kama ndivyo jua ni paka
 
Sifahamu. Mimi nlimpata huku huku awe msaidizi wa home coz sikai sana pale home.
Hizo imani zipo, mimi shambani kwangu pia kuna nyumba na eneo la ekari 4 nimelizungushia fensi ile barbed wire. Nimetafuta pia jamaa na mke wake wanaishi pale huku wakiangalia shughuli zangu. Mara ya kwanza nikaleta mbwa 2 wazuri kweli ili wawasaidie pale. Kweli bwana walikuja kuwa msaada sana na wana banda lao wanatoka saa mbili usiku,yaani pale ilikuwa hakatizi mti. Hata boda boda akitumwa anasimamia mbaliii. Nikaanza kupata malalamiko ya majirani 2 ambao wako mwisho kabisa wa shamba langu, kwamba eti mbwa wangu wanawafukuza mpaka huko kwao. Kuna siku nikaenda kukaa shamba wiki 2 nikagundua ni uwongo maana wale mbwa hawavuki fensi ila ukiingia eneo la mji utaipata. Nikapuuzia, baada ya miezi kadhaa mbwa mmoja akaanza kudhoofika, haraka nikaenda shamba na veterinary, akamcheki weee hakuona chochote, but akampa some antibiotics,lakini after 2 days akafa. Nikiwa safarini nikaambiwa yule mwingine naye kafa ghafla daah. Nikakaa miezi 3 bila mbwa, bahati nzuri Jamaa yangu aliyekuwa anahama akanipa wengine 3 wa saizi nikawapeleka shamba. Baada ya muda wskazoea fresh kabisa, na walivyokuwa wakubwa wao ndiyo walikuwa wakali balaaa, ila hawatoki eneo la hapo home na mtaani hawaendi. Kwa masikitiko nao walikufa mmoja baada ya mwingine, tena anaumwa kidogo then kwisha, yaani sasa sina hata mbwa mmoja. Wakati mjini ninakoishi mbwa wapo miaka nenda miaka rudi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom