yakeshipater
New Member
- Nov 27, 2013
- 2
- 0
Ninasikitika kuwa maafisa wa elimu wote wa manispaa ya Bukoba idara ya shule za msingi wana kiwango cha elimu ya diplama na wengine cheti, wakati wapo walimu tele walio na elimu kiwango cha degree 1 hadi 2 na wana uwezo mzuri wa kuongoza na kuboresha elimu lakini hawapewi nafasi hizo, na mbaya zaidi walimu wa shule za msingi wanapotaka kwenda kujiendeleza kimasomo wananyimwa ruhusa na wale wanaomaliza masomo hata ya diploma ya elimu ya msingi wanalazimishwa kuhamishiwa secondary tena bila malipo yoyote nia yao hawa viongozi ni kukwepa challenges watakazozipata kutoka kwa wasomi hawa. Naomba mnisaidie wadau kwa utaratibu huu tunaboresha elimu au tunabomoa?