JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 2,091
- 4,715
Njoo tukae baa hapa tupate akili ya biasharaHabari wanajukwaa.
Lengo la kuleta uzi huu ni kuomba wazo la biashara ambayo ninaweza kufanya kwa DSM au kwingine, ila pia iweze kuajiri watu wanaonitegemea, kama 4 hivi kwa kuwa maswala ya ajira yamekuwa pia ngumu. Kama nilivyosema mtaji kwa sasa ninayo 10-15milion, lakini pia biashara kama itaanza vizuri naweza kukopa kuongezea mtaji.
Ningependelea biashara ambayo inaweza kuwa na mzunguko wa haraka lakini pia kwa usimamizi sioni tatizo kwa kuwa tayari ninao watu. Nimefikiria muda mrefu kidg sijapata wazo zuri na productive.
Kama kuna sehemu naweza kupata hata maelekezo ya namana kuanzisha biashara kwa vitendo naweza kwenda.
Naombeni msaada jamani kweli hili nipo serious siyo utani. Samahani pia pengine wazo langu sijaliweka vizuri kwa kuwa mie si mwandishi mzuri pia.
Natanguliza shukrani!