Wadau naomba mniambie faida ya nyumba ndogo

The boss, asprin, bishanga na mjomba kaizer ndio wanajua. Kalale ukiamka utakuta majibu.
 
Kisukari kukandia haina maana kuwa si wateja wa hizo nyumba ndogo; lakini ukweli unabaki pale pale madhara ni makubwa kuliko faida. Ni sawa na wavuta sigara; wanajua vizuri madhara yake lakini hawawezi kuacha. lol.

msitudanganye,wengi humu mnajitia kukandia,mkishakutoka jf tu,inakuwa kinyume chake.
 
nyumba ndogo ya nini wakati una kubwa?hata hewa ya kutosha hamna,madirisha madogo kama jela,muda wote unamashaka kama unaoga nje,lol!!
 
Mnanishangaza mnaodai nyumba kubwa kuna stress, ivi nani anaezisababisha hizo stress kama sio mwanaume?Hivi wewe mume kweli usipofanya yale ambayo mkeo hayapendi au yale ambayo ni kinyume na maadili yetu kweli mkeo atakununia? Wake zenu wananuna kwa vile mnafnya ndivyo sivyo!We wahi kurudi home kila siku uone kama mkeo atanuna!

Halafu hivi hamjui kuwa mkeo akinuna watakiwa umbembeleze hadi afurahi?na hayo si ndio mapenzi? Hebu wanaume hudhurieni semina za kidini za jinsi ya kuishi na wake zenu haya yote yataisha jamani!

Nasisitiza, faida za nyumba ndogo HAKUNA!!We mwanaume unaesema zipo unajipa moyo tu na from your heart unaju kuwa unakosea ila tu unajishupaza.

Thanks uloanzisha hii thread
 
wadau wote wa JF katika column hii plse naomba mniambie faida ya nyumba ndogo na kwa nini wanaume walio wengi wanapenda nyumba ndogo,kuna jamaa yangu kaoa juzi tu lakini tayari kwa sasa ana nyumba ndogo

Nyumba ndogo ni rahisi kusafisha hata kama huna mfanya kazi wa ndani. ni cheap kujenga pia maana hutumia matofali machache na cement kidogo. Halafu pia .... eh ... erm ... oh, sorry, nadhani sikuelewa swali!
 
Back
Top Bottom