Wadau nani basi anayeaminika tena kushika hatamu ya uongozi wa Tanzania?

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,142
5,634
Wadau nimekuwa na matumaini makubwa sana na vyama vya upinzani haswa CHADEMA kwa muda mrefu nikiamini huyu ndiye mkombozi ajaye kwa wananchi wa Tanzania. Katika siku za hivi karibuni zimeibuka kashfa za rushwa katika kamati za Bunge, na mbaya zaidi kinachonisikitisha hata wale tunaowaamini sana wa upinzani kumbe nao wamo. Je, kama makucha wameanza kuyatoa mapema namna hii hata kabla ya kushika hatamu kuongoza nchi, wakishikilia nchi itakuwaje?

Ni nani wakumwamini tena basi? Au ndo ule msemo wa "HERI ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA KULIKO ZIMWI LISILOKUJUA" unaanza kujidhihirisha?

Kwa kweli Mbunge yeyote yule wa upinzani aliyekubali kupokea rushwa mmetuangusha mno, hatukutegemea hayo kutoka kwenu.
 
Nchi yeyote duniani haiwezi kusonga mbele pasipo mabadiliko kiuongozi kwa upande wa vyama, cha muhimu hapa changanua kwa makini angalia itikadi za vyama vyote, Sera zao na ili uweze kupata jibu angalia chama kichopo madarakani kina sera gani na kinazifuata sera hizo kiutekelezaji? kwa upande wa Rushwa Chama kilicho madarakani kimeanza kukemea tangu lini na utekelezaji wake ukoje? na hadi leo kiongozi gani ameishahukumiwa kwa kosa hilo. kuhusu CDM labda uwe umetumwa kusema hayo lakini ujue chama imara ukemea maovu na kuchukua hatua, sasa huwezi ukaniambia umepoteza imani wakati haujajua CDM watachukua hatua gani baada ya kuthibitika kuna wabunge wake wamechukua Rushwa kwa CCM tumezoea kusikia wabunge au viongozi wakiwa na kashfa mbalimbali ikiwemo kupokea au kutoa rushwa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
 
Wa kuaminiwa ni Dr Slaa kua rais na pia kuchafuka kwa zitto kusiaribu kuwaamini wapinzani,Kamata mbowe ni muaminifu mtetezi wa kweli,zitto katokea familia ya kimasikini sana huko mwandiga mda mwingi alikua anaoga ziwa tanganyika sasa kaenda bungeni ndio anakusanya kwa rushwa hili nayeye aprove huko kwao kwamba anaweza,zitto ni wa kufukuzwa tu ingawa ndio anatutetea katika SSRA lkn kwa jinsi alivyotuchefua haina hata haja wabunge waaminifu watatutetea hila zitto anaweza tena akatuuza kwa SSRA...Ppppfffuuuuuuuu!!
 
Hapo kwenye red umenena
 
Kweli Mkuu, kwa kweli Dr. Slaa tu ndiye ambaye anaweza kutetea uongozi, but kama watamweka zito nahisi katika hili jambo la rushwa limeshushia hadhi yake sana atakiangusha chama ambacho wananchi wake wameshakiamini sana. Inabidi umakini mkubwa sana katika hili.
 
Mfumo ni priority. Mfumo ubadilike kwanza. Mfumo mzuri utatupatia watu wazuri. Naamini bado wapo.
 
Back
Top Bottom