Wadau nani basi anayeaminika tena kushika hatamu ya uongozi wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau nani basi anayeaminika tena kushika hatamu ya uongozi wa Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanawao, Jul 30, 2012.

 1. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,983
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Wadau nimekuwa na matumaini makubwa sana na vyama vya upinzani haswa CHADEMA kwa muda mrefu nikiamini huyu ndiye mkombozi ajaye kwa wananchi wa Tanzania. Katika siku za hivi karibuni zimeibuka kashfa za rushwa katika kamati za Bunge, na mbaya zaidi kinachonisikitisha hata wale tunaowaamini sana wa upinzani kumbe nao wamo. Je, kama makucha wameanza kuyatoa mapema namna hii hata kabla ya kushika hatamu kuongoza nchi, wakishikilia nchi itakuwaje?

  Ni nani wakumwamini tena basi? Au ndo ule msemo wa "HERI ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA KULIKO ZIMWI LISILOKUJUA" unaanza kujidhihirisha?

  Kwa kweli Mbunge yeyote yule wa upinzani aliyekubali kupokea rushwa mmetuangusha mno, hatukutegemea hayo kutoka kwenu.
   
Loading...