Wadau nadaiwa na M-Pawa Tsh 65,000, kila mara wananitumia sms za vitisho

Box tupo

Member
Nov 2, 2019
55
54
Wadau nadaiwa na m-pawa Tsh 65,000. Kila mara wananitumia sms za vitisho na kuniambia kuniambia kuwa watanichukulia hatua za kisheria.

Cha kushangaza laini yenyewe imefungiwa sababu sina namba ya NIDA.

Je kuna njia nyingine ya kuweza kurudisha huu mkopo wao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki iliyopita nilikuwa mazingira flan, jiran yangu alikuwa ni dada mrembo iv...na sauti ya kibabe.

Aisee, alikuwa anawapiga mkwara hawa wajaa (nadhan ni hao wanaokutisha), moja ya mstari kwenye mkwara wake ilikuwa...''tusitishane kama deni nitalipa sio ujinga, uf...la wa kutishiana tishiana"
 
Hapa tuliowahi kufungiwa laini zetu tushamwelewa mleta uzi, nyie wengine kaeni kimya na mapovu yenu tumieni kuogea mtoe harufu ya shombo la jasho lenu...

TCRA walieleza vizuri kabisa kuwa SMS utapokea km kawaida hasa zile za kukukumbusha kufanya usajili... Sisi tuliofungiwa tukaona kumbe haiishii hapo, had zile unazotumiwa na marafiki, ndugu na jamaa zako unazipokea vizuri tu isipokuwa wakikupigia ndo wanaambiwa namba imezuiliwa kwa muda, na wakitaka kukutumia hela wanaambiwa "mpesa ya mtu mwenye namba hii haipo" (not available)

Na wewe uliyefungiwa, (kwa wale wa voda), huezi jibu sms, kupiga, kutumia data, kuangalia salio, kuingia menu ya mpesa, nk nk nk...

Sasa mleta mada anaogopa vitisho na anataka alipe deni lao ili wasimtishe... Atafanyaje wakati laini yake haipokei wala hairuhusu kutuma pesa?
 
Back
Top Bottom