Wadau mwenye mbinu ya kupunguza fuel consumption kwenye turbo cars anijuze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau mwenye mbinu ya kupunguza fuel consumption kwenye turbo cars anijuze

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Sendeu, May 30, 2011.

 1. S

  Sendeu Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wadau mwenye mbinu ya kupunguza matumizi ya mafuta kwenye magari yenye turbo au cc kubwa kama SUBARU,VX etc naomba anijulishe tafadhali au anishauri
  natanguliza shukrani maana najua hapa bongo kila jambo lawezekana
  tafadhali ushauri uwe wa kifundi zaidi.
   
 2. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Uzoefu kidogo ni air cleaner inatakiwa kuwa safi muda wote, kutokana na vumbi za bongo ikibidi kupiga upepo usisubiri service kama ni muda mrefu may be kila wiki unapulizs gari inakuwa nyepesi.

  Kama ni ya petrol kitu inaitwa miss isiwepo na kuhakikisha plug zinachoma vizuri, la kiuchumi zaidi ni peak hour si busara kuwa barabarani kwa gari hizi, bora uwahi kuamka na kuchelewa kwenda home kama si lazima sana. Kama wakuu wanajua omba flexi time katika kazi.

  Kwa automatic transmission unatumia N wakati wa kusimama katika mataa na kwenye foleni, manual tumia gia ndogo mara nyingi kuanzia tatu na unatingisha kwa kwenye down.

  Kama mtu wa high way speed 90 - 110km/hr ni efficient speed. Umri wa gari pia unamatter
   
 3. S

  Sendeu Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru mdau kwa majibu mazuri hivi turbo ni system inayotumia mafuta sana au? Maana siielewi vizuri hii system msaada zaid tafadhal na kuhusu matumizi ya mafuta hakuna jinsi ya kumodify engine ikawa na matumizi kidogo ya mafuta?
   
 4. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  pole mkuu. Turbo ni kitu inayoendeshwa kwa hewa ya exhaust na kusukuma hewa nyingi kwenye injini na hivyo kuongeza ufanisi wa mashine au injini. Kwa kawaida gari lenye turbo hutumia mafuta kidogo kuliko lisilo na turbo. Mfano landcruiser vx ukilinganisha na gx au standard. Vx ni more fuel efficiency kuliko hizi zingine wakati zote ni 6 cylinder, 4200 cc na zinashare injini ile ile isipokuwa ya vx ilitiwa turbo. Ukija kwenye landcruiser hizo hizo, 200 series zote ni v8 twin turbo 4500 cc, kwa maana ni cylinder nane. lakini ukumbuke hapa nazungumzia diesel engines. Vx gx au base za 200 series zote zina injini ya v8 1vd ftv na zinakwenda hadi km100 kwa lt 10.3 wakati zile za zamani zinakwenda km100 lt 14 au 20mpg. Japo vx ilikuwa economy kuliko zile zingine. Tatizo ni mtengeneza injini aliwekaje mahisabu yake ya wese na si turbo. Turbo inafanya gari kuenda kiurahisi na hivyo kupunguza ulaji wa wese. Nahisi unamiliki subaru ndugu yangu. Pole. Mfano mwingine ni mark 2 baloon 6 cyl inakula lt 1 km 8 wakati benz 6 cyl lt 1 km 13. So, ni mtengezaji kaka. Nunua volkswagen au benz au magari yoyote ya ulaya ni mazuri kwa mafuta sana. Spea ndo noma japo hazifi mapema.
   
 5. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  pia kama ni mpenda mbio uache na kama huachi then wese usilibanie. Hakikisha ule mshale wa mzunguko wa engine hauvuki namba mbili kwa namna yoyote. Gari halitochanganya haraka ila utatumia mafuta vyema. Pia uhakikishe upepo wa matairi uloweka ndo saizi yake na pia aircleaner iwe safi na lisiwe na miss na engine oil ibadilishwe kwa wakati so that the engine is running smooth. Pia usiweke tairi size kubwa kuliko mahesabu ya manufacturer. Hapo utaweza punguza ulaji wa mafuta kwa kiasi fulani. Kama utaweza, zima gari lako wakati wa jam. Joto vipi?
   
 6. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  cha mwisho, jifunzeni ku goole na kupata information za vitu au magari myatakayo. Kama ni subaru ya 2004 kwa mfano, ukiandika 2004 subaru forester mpg utapata forum za kutosha na mambo mengi zaidi ya mafuta utayakuta huko. Wenzetu wananunua magari kwa kuzingatia bajeti zao na anajua kwa mwaka ataghalimikaje kwa mafuta na matengenezo. Nisikuchoshe mkuu. Watakuja wataalam wakupe kitaaluma zaidi.
   
 7. S

  Sendeu Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamii nashukuru kwa elimu mliyonipa vp kuhusu nissan xtrail GT ebu nipeni maana ya hiyo GT na features zake ikiwemo mazuri na mabaya yake nawasumbua ila ndo maana nzima ya kuwa wanajamii
  Asanteni
   
 8. k

  kaliakitu2008 Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka swali lako limenifanya asubuhi hii kufungua google na kisha kutafuta maana ya swali lako na jibu nililopata ni hili: Actually the GT doesn't refer to the engine at all... GT stand for "Gran Tourismo" or "Grand Tourer", which refers to the design of the car. It's a sporty, 2-door saloon. And because it's sporty, the engine is usually a high performance unit.

  kama kuna mwingine anajua zaidi naomba atuletee habari
   
 9. S

  Sendeu Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli nimekubali hapa JF ni zaidi ya kitivo cha Elimu hakika nimeelimika vya kutosha na nashukuru sana kwa michango yenu mwenye mchango zaidi kuhusu topic tajwa tafadhali aulete ili tupate elimu
   
 10. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Habari wandugu, kwanza pole kwa matatizo ya wese ila shaka ondoa mimi nina deal na fuel additives ambapo kwa sasa hivi tumeziingia nchini tanzania zinaitwa F2-21 Fuel Enhancer ambazo kazi yake kubwa ni kupunguza ulaji wa mafuta kwa asilimia mpaka 25% na mchanganyo wake (mixing ratio) ni 1 ltr of F2-21 with 8,000 ltr of fuel (petrol/diesel) kwamantiki ya kwamba 1 litre of F2-21 unaweza kusave mafuta litre 2000 katika kila litre 8,000 hii ni sawa na kusave 2,000 ltres * 2000 Shs per litres = 4,000,000/=. so kama unahitaji napatika kwa namba 0783107531. Our loyal customers are from construction and mining companies. Tunazo package ndogo ndogo kwa wateja wadogo wadogo kama 100ml ambazo utaweza kusafisha mafuta litre 800. Principle behind our product is catalysis. Karibu sana via 0783107531
   
 11. S

  Sendeu Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  madhara yake ni yap mkuu na inawekwa vipi hiyo Fuel enhancer plus cost please tuambie maana lazima itakuwa na madhara kiasi fulani ebu jaribu kutujuza thn tutawasiliana kwa utaratibu huo
   
 12. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hakuna madhara yoyote yatokanayo kwa utumiaji wa hiyo enhancer, na cost yake haizidi dola 400 kwa maana ya laki 6 kwa lita so ukitoa laki sita katika milioni nnne unabaki na faida ya milion tatu na laki nne kama sehemu uliyo save ila sanjari na hilo tuna package ndogo ndogo katika mils 100 ambazo hazizidi dola 45 so kwa small users tunachofanya ni kuweka pacj=kage ndogo kwa mujibu wa matumizi yao ambazo zinakuwa ni chini ya elfu hamsini
   

  Attached Files:

Loading...