Wadau mwendo gani mzuri safarini nisitumie mafuta mengi

kakoyo092

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
720
883
Kama kichwa kinavyojieleza nataka kwenda mwanza kutoka dar nitembee na average ya km ngapi nisile sana mafuta ukubwa wa injini 2.0
Asanteni
 
Mwendo kasi unaua....wewe nenda taratibu speed limit yako iwe ni 60...utafika na utakuwa umetumia mafuta yako vizuri kabisa...haya nenda salama
 
Cha msingi uzingatie alama za barabarani tu ukiona kibao chenye alama ya 50 basi huo ndio mwendo wa eneo husika .

Kwa hakika mwendo unaoshariwa ni mzuri kwa ulaji wa mafuta na usalama wako pia japo wewe hapo umejali zaidi mafuta kuliko uhai wako.

Sio ukanyage kibati mpaka upigwe tochi kisha utakaporudi uanze kulalamika hapa oooh barabarani tochi zimezidi tutakuwa hatuna msaada kwa hilo.

Tii sheria bila shuruti.
 
kwanza inaonekana aunauzoefu na safari ndefu, unachokakiwa kuhakikisha unafanya sheria zote za BARABARA, kuwa makini na vibao na michoro yote ya rod, kama umechoka pata muda wa kupumzika. kwenye speed tembea spedi uliyoizoea (60 mpaka100) ANGALIZO: usitembee na spid ambayo aujaizoea Kwan Gari Inaweza kukushinda na kusababisha ajali
 
Nilienda Iringa toka Dar kwa IST 1.3L nilitumia mafuta ya elfu 40 tu.

Nilichojifunza, uendeshaji unakula sana mafuta tusizingizie gari.

Vitu vya kufanya:

1. Kwanza funga madirisha washa AC acha uwoga.
2. Usiwe na vituo vingi. Kwa 2.0L may be pumzika after every 400km.
3. Acceleration iwe ndogo. Usiondoke kwa vurugu. Yaani acha gari ichanganyie taratibu.
4. Speed nenda 80 to 110kph. Ila kwenye vibao vya 50kph viheshimu. Speed chini ya 80 inakula mafuta na above 120 inabwia mafuta unless una LC V8 4.6L
5. Ila kikubwa ni kua na light-foot. Usiwe na mguu mzito. I mean usikanyage mafuta kama vita. Gusa tu.
 
kuendesha taratibu kupita kiasi ni kosa kisheria mfano maeneo ambayo gari zipo more than 70kph we uko na 40 katikati ya barahara pia ni kosa pia ..

BUT

gari nyingi at 80kph zinatumia mafuta kidogo kuliko spid yeyote ile ukizid mafuta yanazid pia ukipunguza mafuta yanazidi

weka 80 ufurahie maisha ila utalala njiani au kufika usiku wa manane
 
Hapo ni mchezo wa RPM ( rotation ) 2 to 2.5 ikizidi ina kula mafuta na ikipungua nayo ni tatizo kingine accelator usiikandamize wewe iguse tu
 
Mkuu hakikisha usiendeshe chini ya 120 hapo utatumia mafuta ya 10000 dar to moro (jokes)
Sina uzoefu na magari nilipenda tu kuchangia uzi huu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom