Wadau msikieni Mary Nagu anavyo lialia na nyie Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau msikieni Mary Nagu anavyo lialia na nyie Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Oct 21, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, amewataka Watanzania kuacha tabia ya kulalamikia uwekezaji na badala yake wauone chachu ya ukuaji wa uchumi wa nchi na ustawi wa jamii.
  Waziri Nagu amesema hiyo inatokana na uwekezaji kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji uchumi na utoaji wa ajira kwa watanzania.
  Aliyasema hayo jijini hapa jana baada ya kutembelea Kiwanda cha Bia nchini (TBL), tawi la Mbeya, viwanda vya kuzalisha zana za kilimo, kiwanda cha kutengeneza vifaa vya ujenzi na vya majumbani cha Marmo Granito Mines (T) Ltd.
  Aliwataka Watanzania kutambua umuhimu wa uwekezaji maana uchumi wa nchi sasa unakua kwa kiwango kikubwa kutokana na uwekezaji huo.

  Dk. Nagu alisema pasipo uwekezaji pato la taifa haliwezi kukuzwa, kupata ajira na kupata bidhaa mbalimbali.
  Akiwa katika kiwanda cha kutengenezea vifaa vya majumbani na ujenzi cha Marmo E Granito Minest (T) Ltd pamoja na kwamba wana asili ya Asia lakini ni Watanzania wamewekeza huku wakitumia malighafi za hapa nchini kutengeneza bidhaa mbalimbali.
  Aliwataka Watanzania kujenga tabia ya kuweka akiba ya mapato yao ili yaajiri na wanaosaidia kukuza uchumi wa nchi.
  Hata hivyo, Waziri Nagu aliutaka uongozi wa kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ambacho kilibinafsishwa na kubadilishwa matumizi yake, kujiandaa kuanza kutengeneza zana hizo mara chuma cha liganga na Nchuchuma kuanza kufanya kazi ya kuzalisha chuma.
  Alisisitiza kuwa asingependa kuona kiwanda hicho kinaendelea kuwa ghala la bidhaa kutoka nje ya nchi kama ilivyo hivi sasa bali wajiandae kuanza kuzalisha zana za kilimo na pembejeo kama awali.

  Akiwa TBL tawi la Mbeya, Dk. Nagu alisema kiwanda hicho kimewekeza zaidi ya Sh. bilioni 82 na kinatumia mazao ya ngano na shayiri ambayo yanazalishwa hapa nchini ambapo taifa linapata kodi na Watanzania wengi wamepata ajira.
  Alisema mazingira hayo yamepatikana kutokana sera nzuri ya uwekezaji ambayo inavutia wawekezaji kutoka nje ambao wanahitajika na mataifa mbalimbali duniani lakini wamekuja nchini na matunda yake yanaonekana na kila Mtanzania.
  Waziri Nagu alisema Nyanda za Juu Kusini sasa ni wakati wake katika uwekezaji na ina vivutio vingi.
  Alivitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa ni kilimo, madini, utalii na kuwataka watu wafanye kazi kwa bidii ili kupata mitaji na kuwekeza kwa lengo la kusaidia kujiletea maisha bora.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Raymond Mbilinyi, alisema Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini umeiva kiuwekezaji na kuzinduliwa kwa kituo cha TIC itakuwa ni chachu ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kufurika kuwekeza.
  Alisema kituo hicho kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali, watahakikisha changamoto zote zinazorudisha nyuma shughuli za uwekezaji katika ukanda huo zinafanyiwa kazi ili kutoa fursa zaidi za uwekezaji.
  Meneja wa TBL tawi la Mbeya, Calvin Martin, alisema kiwanda hicho kinafanya vizuri na uzalishaji umekuwa ukiongezeka kwa kasi na kimekuwa kikitoa ajira kubwa kwa jamii na misaada mbalimbali kwa jamii katika shule, hospitali, usafi wa mazingira na michezo.
  Alisema kiwanda hicho cha Kanda ya Mbeya, kinahudumia mikoa ya Ruvuma, Iringa, na Rukwa na mauzo yake yamekuwa yakikua kila mara.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hatukatai uwekezaji ila tuna pinga namna ya mgawanyo wa umiliki katika uwekezaji!
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Naona siku hizi hawamwiti tena Dr.Mary Nagu kuna kitu wameshitukia nini ?
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  He he he doktoreti feki wako wengi hawa-Nchimbi, Mahanga

  uwekezeji mzuri uwe unahusisha jamii husika na maslahi yake yaani uwe na uwazi na iwe rahisi kufuatilia
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  kwanini hii serikali isiamue kumpawa mzawa kuliko kutuletea hayo manyonya damu?
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  People remain cynical about foregn investors and the whole concept of privatisation because it has been on their own disadvantage. We have recently witnessed unnecessary disputes between wananchi and investors over land ownership and the government sides with those investors to oppress its own people. Additionally, FDI hasn't yet translated itself into provision of relief to a number of people's problems but only serves to profit a select group of leaders who benefit through those exploitative contracts they sign.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Unajua hawa viongozi wetu wanadhani wanaongoza watu wasio na akili,hivi ni nani anayepinga wawekezaji wale wa ndani na nje? Tuache kupindisha hoja hapa,tatizo la msingi ni namna wanavyogawa rasilimali zetu...Wanatumia njia mbalimbali kualalisha uovu wao.....tunataka mgawanyo ulio wa haki,nchi ifaidike na wananchi wanufaike kwa kuzaliwa Tanzania...tuone tofauti ya kuzaliwa Somalia na kuzaliwa Tanzania ati!!! Kwasasa inafikia kipindi unalaumu kwanini ulizaliwa kwenye nchi ya ajabu namna hii....bureee kabisaaa...
   
Loading...