Wadau, JK kafika Same? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau, JK kafika Same?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Brooklyn, Nov 16, 2009.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu kuna jambo linanitatiza kidogo, nimemuona mkuu wa Kaya over the week end mitaa ya mlimani city ambako pamoja na mambo mengine naambiwa kulikuwa na show ya wanamuziki fulani wa kutoka nje ya Kaya, na kwa taarifa nilizozipata jana sasa yuko Italia!!

  Lakini sijasikia kama alipita pale Same kuwapa pole ndugu zetu waliokumbwa na msiba mzito!!

  Wadau mtanisahihisha if I'm wrong!!
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  Bwa-ha hahahahhahhahahha
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni, nilipata habari za msiba wa Same (niko nje ya Tz) . Nikasikitika sana. Sasa ninashangaa zaidi mnaposema mkuu wa kaya hakufika pale. Yes, hii siyo priority yake. I hope mama Anna Kilango-Malecela was there!!!! Nafikiri kwa vita inayoendelea kusafisha richmond na mafisadi ambapo kuna direct attack kwa wanaovalia nzuga masuala haya basi mkuu wa kaya hataweza kwenda kinyume na msimamo wa Sophia Simba (puppet mkubwa huyu). Sorry to say this. Ila sasa kwa wapiga kura wa Same bado mtaendelea kumchagua Rais CCM??? Kwa mbunge is ok. Naombeni mpunguze zile kura za sunami za 2005.
   
 5. J

  Jahom JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kaya ilipeleka misaada, iwapo angeenda gharama ingekuwa kubwa.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  JK alionekana kule kwa Msoga baada ya watu wa kijiji ambapo ni asili yake kukumbwa na maafa ya nyumba zao kuezuliwa mapaa baada mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha nyumba nyingi haswa zile za mbavu za mbwa kuanguka... kesho yake akapaa Italia...
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,273
  Likes Received: 22,030
  Trophy Points: 280

  dahh...
  Kwa hiyo same hawezi kwenda kuuza sura.
  Au huko ndio kuna mahandsome zaidi ameogopa atafunikwa?
  Mkuu wa kaya kachemsha...
  Angeenda kuwapa pole wafiwa badala ya kukimbilia pasta na pizza italy
   
 8. B

  Bobby JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  hivi JK ni mbunge au rais? Maana kwa records zangu hakuna aliyefariki Bagamoyo lakini Same tumewapoteza zaidi ya Watanzania 20. Anyway mimi c wa usalama wa Taifa huenda wao wanaweza kutupa jibu zuri zaidi ktk hili lakini common senses zetu wengi zinashindwa kumuelewa kabisa huyu baba wa Bagamoyo. Vitu ambavyo siku zote tunajuwa ni priorities kwake ni completely sio priorities na vile ambavyo ni upuuzi wa kutupwa kwake ndio priorities.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa Kaya leo yuko Roma, Italia. Ndugu wa Same wasubiri kidogo.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Rais alituma rambi rambi kama sikosei suala la yeye kwenda nadhani lilitegea ratiba yake kama ingeweza kuwa na upenyo na ikizingatiwa kwamba tangu tukio la mwanza siku hizi ratiba yake imebadirishwa na hafanyi ziara ambayo watu wake hawaja ipanga.

  Wa kulaumiwa hapa ni ofiya yake inayohusika na ratiba pamoja na kwamba na yeye hakuwa na hamu ya kwenda huko. Pia ki-usalama huwezi kumpeleka rais wa nchi mahali ambapo usalama wake hauna uhakika na haikujulikana mara moja nini kimesababisha mlima kuporomoka so si rahisi watu wake wa usalama kumruhusu aende huko.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teh teh alikuwa anajipiga facial na mapoudaaa kujianda kwenda Italy nadhani ataunganisha juu kwa juu kwenda mapka jamaica....ndugu zangu wa Same poleni.msijali mtamuona na atakuja wakati wa kampeni 2010
   
 12. Companero

  Companero Platinum Member

  #12
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Delagatus non potes delegare!
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Alikwenda kwao Msoga kuangalia kama makasili anayojenga yalinusulika na upepo; muungwana priorities zake anazijua mwenyewe na ndio maana ana mawaziri kwenye cabinet yake wana vyeti vya kufoji lakini hashstuki hata mara moja; mambo kama hayo hayamyimi usingizi eti!!Jamani imekula kwetu hiyo!!
   
 14. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145

  This is ridiculous!! Gharama ipi kubwa mzee?? Kwenda Monduli kwenye bethidei ya EL na pale same kwa wafiwa???


  I strongly believe Mkuu wa Kaya had moral reasons to console these poor Tanzanians let alone viroba vya unga ambavyo hata sisi walala hoi tumepeleka!!
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Same ndo Anne Kilango??? huyu mama si ndo anadai bungeni patachimbika kama TICTS, Richmond, meremeta hazitashughulikiwa au??

  Na anavikashifa tuvyake vya nanihinooo ***kulevyaaa...wamemsitiriiiiii!!!!
  Naona mkuu wa kaya ratiba ilikuwa tight tayari akaamua aelekee hapoo karibu home bmoyo kutoa poleee....

  Same kuna huyoo Anne, John, RC wa Knjaro tena kwa niaba ya Raisi walimwakilisha vilivyooo mkuuu..Hata baadae utamsikia mwenyewee Anne akimshukuru mkuu wa kaya kwa serikali kutoa msaada wa hali na mali kama Mwenzie Sendeka,Sita,Seleli na Mengi wanavyomwita Mkuu ndo Kamanda wa Vita ya Ufisadi...
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Anaweza kuwa alijisikia kizunguzungu alipotaka kwenda Same. Akashauriwa apumzike. Nimesikia akitoka Roma atakuwa pale uwanja mpya kupokea kombe la dunia (hata sijui tumeshinda lini kombe hili!).
  Atakuwa na akina AY, Nameless, Babra Hassan, Gerald Hando,......
   
 17. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145

  Nchi hii tuna tatizo katika kujua vipaumbele kwa watu wetu!! Wakati ikiripotiwa kwamba watu wanashindia ubuyu kila siku kwa kukosa chakula hapo Dodoma, 'yeye anaenda kupokea kombe la dunia'.

  Naamini wapanga ratiba ya Mkuu wa Kaya hawaishi Tanzania!! Hata kipofu anaona matatizo tuliyonayo, kila kona ya nchi hii kuna vilio. Nani wa kuwasikia masikini hawa?

  Ningelikuwa mimi ningesitisha safari za nje ya nchi angalau kwa mwaka mmoja nifuatilie matatizo ya wapiga kura wangu!!!
   
 18. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Alikuwa busy akiserebuka mlimani city. That is his priority.

  Kwa viongzi wetu sio jambo la kushangaza. Kumbuka wakati ule wa mwinyi kulikuwa na mgomo muhimbili na walitaka kuonana na rais lakina wakasema raisi hana nafasi na wakati huohuo wa mgomo akaenda Uwanja wa taifa akawa anacheza "Isambe" wakati wa onyesho la mwanamuziki wa congo kanda bongo man huku watu wakifa ovyo muhimbili. Shame to africans

  What matters is the priority of a president and not the priorities of a nation
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jamani lazima mkubali Rais ni mmoja na nchi ni kubwa sana. rais ana shughuli nyingi sana za kitaifa, kimataifa na hata zake private.

  Ameteua baraza lake la mawaziri na kuwapa task mbalimbali kama wawakilishi wake.

  Sipo Tanzania. lakini nina imani kubwa Mkuu wa mkoa atakuwa amefika na vile vile Waziri au mawaziri wake watakuwa wamefika katika eneo la tukio.

  Mkuu wa mkoa, mawaziri na hata makamo wake hao wote ni wawakilishi wa Rais na wanafanya kazi kwa niaba ya rais.

  La muhimu ni kuwasaidia wale waliopata majanga na kuhakikisha maiti zinapatikana na kuzikwa kwa mujibu wa imani zao
   
 20. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 779
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 80
  Mkuu wa kaya ni muuza sura mzuri kwenye nchi za watu, hivi hizo ziara zake zimeleta kitu gani ambacho ni tangible cha kujivunia. Mi nilimsikia (tena kwa kujilazimisha kusikia hotuba zake siku hizi) eti wananchi wajenge nyumba imara za matofali ya kuchoma, cha kushangaza sijui ni kwa vipi amewawezesha kufanya hivyo..Masikini same! masikini TZ
   
Loading...