Wadau, je neno "laana "huwa ni kiumbe chenye uhai

Speed of light

JF-Expert Member
Nov 8, 2014
313
284
Mara kadhaa utasikia watu wakisema fulani ana laana ya wazazi au ardhi hii imelaaniwa au utasikia umoja wa mataifa umeilaani nchi fulani , wakati mwingine utamsikia mtu akilalamika pekee yake huku akijiuliza 'hivi mimi nimelaaniwa...? ni kwanini nakutana na mikosi kila mara .

Wadau laana ni kitu gani hasa...?
Je mikosi ni sehemu ya laana.. .?

Je" laana" ni kiumbe chenye kumfuata aliyelaaniwa kila mahali kwa lengo la kumharibia mambo yake.? kumfikishia musuko suko, ajali au hata kumharibia kazi,biashara zake....? laana ni kitu gani hasa...?
 
Laana ni manung'uniko ya dhati toka upande mmmoja kwenda mwingine...mzazi kwa mtoto..mtu kwa mtu n.k

Chagizo kubwa ni kuwe na nung'uniko la dhati..ndo maana kama mtu hajaonewa na hakuna lalamiko LA dhati basis ni ngumu kumlaani mtu.
 
Mmh ewanajamvi wengi humu hua wanasema Tanzania tumelaaniwa! Ngoja wataalam waje wa laana
 
Laana ni manung'uniko ya dhati toka upande mmmoja kwenda mwingine...mzazi kwa mtoto..mtu kwa mtu n.k

Chagizo kubwa ni kuwe na nung'uniko la dhati..ndo maana kama mtu hajaonewa na hakuna lalamiko LA dhati basis ni ngumu kumlaani mtu.
Sasa kama kweli unakosa na mtu mwingine akakuandama na wewe ukanung'unika kwa dhati hiyo nayo ni laana ilhali kosa umefanya kweli
 
Mara kadhaa utasikia watu wakisema fulani ana laana ya wazazi au ardhi hii imelaaniwa au utasikia umoja wa mataifa umeilaani nchi fulani , wakati mwingine utamsikia mtu akilalamika pekee yake huku akijiuliza 'hivi mimi nimelaaniwa...? ni kwanini nakutana na mikosi kila mara .

Wadau laana ni kitu gani hasa...?
Je mikosi ni sehemu ya laana.. .?

Je" laana" ni kiumbe chenye kumfuata aliyelaaniwa kila mahali kwa lengo la kumharibia mambo yake.? kumfikishia musuko suko, ajali au hata kumharibia kazi,biashara zake....? laana ni kitu gani hasa...?

Hivi wewe huna kamusi?? Au unataka kutusumbua tu
 
Hivi wewe huna kamusi?? Au unataka kutusumbua tu
Hapa jf hatusumbuani, bali tunaelimishana na kuhabarishana yale unayoyajua huenda mwingine hayajui na kamusi inatoa ufafanuzi usio kidhi kiu ya mhitaji ,ndio maana nikaja hapa jf ili kupata angalau zaidi
 
Hivi wewe huna kamusi?? Au unataka kutusumbua tu
"Ningekuomba upitie kasehemu haka nilikakuta mahali nikaisoma sikupata jibu bali ilinizidishia shauku ya kutaka ufahamu zaidi"

Kama tukingali hapa duniani, tutaendelea kukumbana na matukio kadhaa ya Kupata au kuishiwa, kufarahi au kuhuzunika, kuoana au kuachana kwa sababu za kifo, kuwa na wanawake tasa, kuwa na wanawake wanaotokwa mimba, tutaendelea kuwa na watu maskini, tutaendelea kuwa na viongozi wanaotusababishia Laana bila sisi kutaka, tutaendelea kuwa na ukame, mafuriko na vimbunga, tutaendelea kuwa na mafisadi, nk. Hayo yote ni LAANA ambazo zitaendelea kutuzunguka pande zote hata kama Tumeokoka. LAANA ZINGINE HATA UNGEFUNA NA KUSALI HAZITOKI KATU.
Naomba nimalizie kwa kuzungumzia LAANA zitokananzo na wazazi wetu. Chukulia mfano wa Mzazi ambaye alikataa kumpeleka mtoto wake kusoma shule kwa sababu tu aliona mtoto wa kike hana faida yoyote kumpeleka shule. Mtoto huyu atakuwa hajui kusoma wala kuandika. Mtoto huyu atakuwa hawezi kusoma Biblia wala maandiko yoyote ya Mungu. Mtoto huyu atakuwa hawezi kufanya Biashara na mahesabu ya pesa yatamshinda kwa sababu hakusoma. Matokeo yake kwa kutokusoma ATAAMBULIA KUWATUMIKIA WATU WENGINE TU MPAKA KUFA KWAKE. ATASHINDWA KUINUKA KIUCHUMI AU KIMAISHA KWA SABABU TU HANA ELIMU. Hii bila shaka itakuwa ni LAANA ambayo imesababishwa na maamuzi mabovu ya Mzazi. Mtoto huyu atashindwa kulima kilimo cha kitaalam, Mtoto huyu atashindwa kuendesha familia yake na kuiwekea misingi ya kudumu kiuchumi. Watoto wa mtoto huyu na wajukuu wake huenda wote wakawa Hohe Hahe kiuchumi na Kijamii kwa sababu tu Babu wa Mzazi wao alifanya maamuzi ya kutompeleka shule mtoto wake. LAANA ya mfano huu mwenye uwezo wa kuiondoa ni mamlaka ya nchi husika (Serikali) inayoweka sera mathubuti ya kuhakikisha kila mtoto anasoma mpaka ngazi ya mwisho ya shule mzazi wake apende au asipende.
 
Back
Top Bottom