Wadau huu ni ugonjwa gani wa Kuku na unatibiwaje?

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Wadau vifaranga wangu wanaumwa midomo na macho! Inaanza kwa kutokea manundu manundu hadi yanaziba macho kama muonavyo! Naomba kujuzwa huo ni ugonjwa gani? Dawa za kuutibu ni zipi!

IMG_20210413_064810.jpg

IMG_20210413_064839.jpg

IMG_20210413_064831.jpg
 
Nenda kwenye maduka ya dawa za mifugo ulizia chanjo mpya inaitwa moja tatu. Ila hao ambao wameshaugua huwezi kuwaponesha kwa kuwapa chanjo.
 
Asante sana kwa ushauri mzuri! Hiyo chanjo hilo ndiyo jina lake,yaani moja tatu?Pia nini kifanyike kwa hao wagonjwa pamoja na kwamba unasema kwa sasa chanjo haiwezi kuwaponya?
 
Yes moja tatu ndio jina la chanjo. Kuhusu hao wagonjwa uwezekano wa kufa ni mkubwa kuliko wa kupona ila jaribu kuchanganya punje za mahindi na mafuta ya kula kisha uwape, siwezi kukuhakikishia kuwa ni dawa ila unaweza kujaribu.
 
Aksante sana mkuu ngoja nijaribu
 
Wapatie antibiotics pia wapake mafuta (vaseline au mafuta ya kula) pale inapowezekana kwenye hivyo vinundu. Hii ni mbinu tu ya kupunguza vifo na kutibu side-effects za ugonjwa.
Naunga mkono hoja
wakamue pale unapoweza, wapake Vaseline hii huzuia hewa isipite na hivyo kwa kiasi kikubwa hawa Virusi hufa.
Antibiotic pia ni muhimu na ukikosa wape maji ya alovera kama mbadala
J
 
Yes moja tatu ndio jina la chanjo. Kuhusu hao wagonjwa uwezekano wa kufa ni mkubwa kuliko wa kupona ila jaribu kuchanganya punje za mahindi na mafuta ya kula kisha uwape, siwezi kukuhakikishia kuwa ni dawa ila unaweza kujaribu.
Ulichosema ni ukweli mtupu wale vifaranga asilimia 95%macho yamevimba na hawaoni tena!Asilimia 4,wamekufa!😥😥😥
 
Koroga sabuni kwenye maji masafi,then wasafishe na mapovu sehemu kwenye uvimbe..pia hakikisha mapovu yanaingia ndani ya macho.
Baada ya siku tatu utakuja kunishukuru,mara nyingi hayo ni magonjwa yanayotokana na bakteria,so sabuni inatabia ya kuuwa bakteria..mimi ndio dawa ninayoitumiaga .
 
Asante!Ngoja nijaribu,nitakupa mrejesho!
 
Koroga sabuni kwenye maji masafi,then wasafishe na mapovu sehemu kwenye uvimbe..pia hakikisha mapovu yanaingia ndani ya macho.
Baada ya siku tatu utakuja kunishukuru,mara nyingi hayo ni magonjwa yanayotokana na bakteria,so sabuni inatabia ya kuuwa bakteria..mimi ndio dawa ninayoitumiaga .
Huo ugonjwa unasababishwa na virus sio bacteria ndio maana hauna tiba bali una chanjo, hizo mbinu nyingine za matibabu ni kama ramli tu.
 
Nenda kwa wizara ya afya ya wanyama watakupa dawa, ila next time wape dawa ya ndui ya chanjo wakiwa vifaranga, omba mafunzo ya watalam
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom