Unalionaje suala la jamii kutaka mtu aishi wanavyotaka wao?

Boeing 757

JF-Expert Member
May 18, 2020
288
612
Unajua katika ulimwengu wa leo kuna lifestyle za kila aina. Na pia kila mmoja hupendelea kufanya kile apendacho. Ila kuna hali fulani ninaiona kwenye jamii hususan inayonizunguka.

Ipo hivi; Kama wewe ni kijana labda tuseme kuanzia 20+yrs kama huzinyoi kwa style za kisasa au kutengeneza nywele zako kama kusokota dreads, nywele zako zipo kawaida tu kama zilivyo. Yaani unaonekana mtu wa ajabu sana.

Pia kama upo single hauna muda wa kukimbizana na sketi, sio mtu wa totoz lazima watakutolea kashfa, mara ni hanithi mara ni domo zege (japo yaweza kuwa inachangia). Wanakuona kama umepitwa na wakati na ni mshamba wa mwisho.

Na pia kwa mfano ukipita hata barabarani na kitabu hata cha story labda umekiazimisha mahali unapita nacho umekibeba mkononi lazima watakushangaa kinoma kana kwamba ni kitu cha ajabu sana.

Yapo mambo mengi sana kwenye jamii inayonizunguka nayaona hayapo sawa lakini hebu nisaidieni haya machache.

JE, JAMII YETU KUNA KITU GANI HAKIPO SAWA AU NI MHUSIKA MWENYEWE KWA HAYA MASWALA HAYUPO SAWA?
 
Maisha ni kusengenyana, kumsema mtu, na wew kusemwa na watu, ila mradi usimuumize wala kumjeruhi mtu.
 
Ukifata sana watu wanavyokuona yatakukuta mabaya sana, maana sasa hivi kuna watu wameharibikiwa hadi wanalilia haki zao.

Fata yako utashinda mengi
 
Binadamu huyatafsiri maisha kulingana na tamaduni au mazoea aliyokuziwa na wengi wao wasiokuwa na upeo zaidi ya waliokuzwa nao huwa wanafikiri maisha wanayoishi wao ndio maisha ya kila mahali na kila mtu.
 
Fikiria unachotaka kufanya duniani kuiongezea historia dunia. Wajinga wajinga potezea

I can calculate the motion of heavenly bodies, but not the madness of people.

Isaac Newton
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom