Wadau! Hebu tulitazame kama ni kweli ni tabia ama desturi wetu! Sijawahi kuona!!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Je? Ni sahihi kwa tabia na desturi yetu Watanzania kwa Mwanamke kumhalalisha mnyama yeyote na hata kuku? Hili nimeliona jana katika pilikapili ya kuufurahia mwaka mpya kwa jirani zangu mwanamke akilazimishwa na mumewe kuhalalisha kuku kwa ajili ya kitoweo na mwanamke alikataa katukatu na akidai tangu azaliwe hajawahi ona mwanamke akitenda hili.

Wadau! Je? Huyu mama alikuwa sahihi kukataa??
 
kwa wakristo ni halali kwani kinachotakiwa na kilichoandikwa ni mnyama achinjwe lakini kwa waislamu hairuhusiwi mwanamke kuchinja lbd ikibidi km hakuna jins.
 
Kumhalalisha sijui unamaanisha nini?

Ila kama ni kuchinja, ukija kwangu ukala kuku
100% jua nimechinja mwenyewe

Mwanamme haitwi kuchinja kuku
Labda ng'ombe, mbuzi, kondoo ndo vyachinjwa na waume.

Tangu utotoni nachinja kama kawa, tna na kumkimbiza nakimbiza mwenyewe.

Hiyo ni tamaduni za ulikotoka tu.
 
Kwako Kongosho:

Kuhalalisha & Kuchinja,kuna tofauti ktk uwelewa wako? Naomba ufafanuzi angalau!
 
Kumhalalisha sijui unamaanisha nini?

Ila kama ni kuchinja, ukija kwangu ukala kuku
100% jua nimechinja mwenyewe

Mwanamme haitwi kuchinja kuku
Labda ng'ombe, mbuzi, kondoo ndo vyachinjwa na waume.

Tangu utotoni nachinja kama kawa, tna na kumkimbiza nakimbiza mwenyewe.

Hiyo ni tamaduni za ulikotoka tu.

FF uko wapi leo? Kwamba 100%...?
 
nilikuwa naioshi arusha nikapata tenda ya kusupply kuku EA HOTEL YAANI WALE WASOMALI WALIKUWA WANAHESABU PINGILI KWENYE SHINGO KUCHEKI KAMA NIMENJINJA MWENYEWE
YAANI KUKU MIA NNE ANAHESABU MMOJA MMOJA JAMANI
WAISLAMU WANACOMPLICATISHA SANA HII MAMBO
 
Mashauzi tu!
Mbona soseji wanakula, wana uhakika kama hao ng'ombe wamechinjwa na Waislaam?
 
andare,
Pale Arusha meat hakika ninasema ukweli maana pale nimeshafanya kazi takrban miaka 6
Pale kuna Mashehe zaidi ya watatu ambao bodi ya Arusha meat imekaa na kuwachagua kuhakikisha wanahalalisha chochote kiitwacho mnyama atakechinjwa pale.
Na hili limefikiwa na bodi yote baada ya Wakirsto na Waislamu kukaa na kuafiki ya kwamba iwe hivyo,na Wakirsto walikubali iwe hivyo kwa sababu wao hawafungamani hata kidogo na wakiwa na IMANI ya kwamba yote ni Kheri tu na walitakiwa kuwepo na mchanganyiko ktk wahalalishaji Wakirsto wakasema wao wana Imani na waachiwe Waislamu wawe wanahalali kusudi wajue ya kwamba Wakirsto wao wana Imani waweze kula bila ya hofu yeyote.

Na siyo kwmb unaonaga mtaani tunamtafuta Muislam atuhalalishie ukafikiri Wakirsto hawawezi ni kwmb tunataka hata akifika kwako muda ule aweze kushiriki nawe kwa chochote ulichoandaa.
Hbr ndiyo hiyo.
 
Kumhalalisha sijui unamaanisha nini?

Ila kama ni kuchinja, ukija kwangu ukala kuku
100% jua nimechinja mwenyewe

Mwanamme haitwi kuchinja kuku
Labda ng'ombe, mbuzi, kondoo ndo vyachinjwa na waume.

Tangu utotoni nachinja kama kawa, tna na kumkimbiza nakimbiza mwenyewe.

Hiyo ni tamaduni za ulikotoka tu.

ha ha ha mwanamke mjeiri wew sijapata kuona!! kah
 
andare,
Pale Arusha meat hakika ninasema ukweli maana pale nimeshafanya kazi takrban miaka 6
Pale kuna Mashehe zaidi ya watatu ambao bodi ya Arusha meat imekaa na kuwachagua kuhakikisha wanahalalisha chochote kiitwacho mnyama atakechinjwa pale.
Na hili limefikiwa na bodi yote baada ya Wakirsto na Waislamu kukaa na kuafiki ya kwamba iwe hivyo,na Wakirsto walikubali iwe hivyo kwa sababu wao hawafungamani hata kidogo na wakiwa na IMANI ya kwamba yote ni Kheri tu na walitakiwa kuwepo na mchanganyiko ktk wahalalishaji Wakirsto wakasema wao wana Imani na waachiwe Waislamu wawe wanahalali kusudi wajue ya kwamba Wakirsto wao wana Imani waweze kula bila ya hofu yeyote.

Na siyo kwmb unaonaga mtaani tunamtafuta Muislam atuhalalishie ukafikiri Wakirsto hawawezi ni kwmb tunataka hata akifika kwako muda ule aweze kushiriki nawe kwa chochote ulichoandaa.
Hbr ndiyo hiyo.

thanks kwa maelezo mkuu.
Nilikuwa sifahamu hayo...
 
Back
Top Bottom