Wadau bandari wachachamaa kukatika umeme 'Long room' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau bandari wachachamaa kukatika umeme 'Long room'

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Jan 20, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 85,194
  Likes Received: 60,492
  Trophy Points: 280
  Wadau bandari wachachamaa kukatika umeme 'Long room'


  Na Mwandishi Wetu

  WADAU mbalimbali wa bandari nchini wameiomba serikali kuhakikisha Idara ya Ushuru wa Forodha inapewa kipaumbele katika tatizo la sasa la mgawo wa umeme kutokana na umuhimu wake kwa uchumi wa taifa.Wakizungumza kwa
  nyakati tofauti jana, wadau hao walieleza kusikitishwa na taarifa za kusimama shughuli katika eneo hilo nyeti kutokana na matatizo ya mgawo wa umeme.

  Baadhi ya vyombo vya habari jana viliripoti kuwa wateja na wafanyakazi wa Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya Ushuru maarufu kama 'Long room' jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita ililazimika kusitisha shughuli zake baada ya jenereta iliyokuwa ikitumika eneo hilo kupata hitilafu wakati eneo hilo likiwa kwenye mgawo wa umeme.

  Akizungumzana gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA) Bw. Emanuel Mallya alisema ni kosa kubwa eneo nyeti kama hilo kwa uchumi wa nchi kuwa na umeme wa kubahatisha.

  Alisema kuwepo jenereta ya tahadhari eneo hilo si suluhisho kinachopaswa kufanyika ni serikali kuhakikisha inalilipa hadhi eneo hilo kati ya yale nyeti ambayo hayapaswi kukosa umeme kutokana na umuhimu wake.

  "Mchakato wote wa kutoa mizigo bandarini unaanzia Long room, documents (nyaraka) zote za wateja zinasukumwa kwa komputa hapo Long room. Kukosekana umeme eneo hilo maana yake ni kusimama kwa mchakato mzima wa shughuli za bandari ambalo ni lango kuu la biashara na tegemeo la mapato ya nchi," alisema Bw. Mallya.

  Alifafanua kuwa kwa siku moja, taifa linakusanya zaidi ya sh. bilioni 5 kutoka kitengo hicho huku akitoa mfano kuwa kitendo cha juzi kukosekana umeme eneo hilo, kilisababisha hasara kubwa kwani makusanyo yalikuwa karibu sh. milioni 400 tu.

  "TRA inafanya kazi nzuri sana, siilaumu katika hili hata kidogo! Ushauri wangu ni kuitaka serikali kutambua kuwa sehemu ya Forodha ni roho ya mapato ya nchi, hivyo kama maeneo mengine nyeti mfano hospitali kubwa, jeshini nk. lisiwekwe kwenye mgawo wa umeme. Long room inapokosa umeme tunapoteza mabilioni yanayohitaji kuendesha sekta zingine za maendeleo ya nchi," alisema mwenyekiti huyo.

  Alifafanua kuwa tatizo hilo linaweza kuzua mambo mengine kwa kuwafanya wateja wa nchi jirani wanatumia Bandari ya Dar es Salaam kupitisha bidhaa zao nchi zingine ili kuepuka hasara zitokanazo na kucheleweshwa mizigo yao.

  Aliongeza kuwa kuchelewa kuchukua mizigo kunakwenda sambamba na ongezeko la gharama hivyo kusisitiza kuwa njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ni kuhakikisha linakuwa na umeme muda wote.

  "Tunaposema mgawo maana yake, tunakuwa na umeme usiotosheleza mahitaji hivyo unagawiwa maeneo mbalimbali kwa muda maalumu. Tuna maeneo ambayo kutokana na unyeti wake yanapata umeme muda wote mbali ya matatizo haya. Naiomba serikali itoe kipaumbele hapo Long room ambapo karibu asilimia 95 ya mapato ya nchi kwa kutwa yanapatikana," alisema na kuongeza;

  "Kutokana na teknolojia ya sasa ya mawasiliano ya kompyuta mfumo wa nchi nzima wa forodha umeunganishwa pamoja sehemu moja hivyo umeme kukosekana Long room nchi nzima inakosa makusanyo yakiwemo maeneo ya vituo vya mipakani.Aliomba Wizara ya Fedha na Uchumi, Nishati na Madini na ile ya Uchukuzi kukaa pamoja kuona umuhimu wa eneo hilo nyeti kwa uchumi wa nchi na kuhakikisha linapata umeme.

  Naye Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw. Otieno Igogo alisema eneo hilo kuwekwa kwenye mgawo ni tatizo kubwa lakini liko ndani ya uwezo wa nchi na linaweza kutatuliwa haraka.

  "Idara Forodha ni muhimili wa uchumi wa nchi kitendo cha umeme kukosekana Long room Jumatatu kilisababisha kitengo hicho kukusanya asilimia 10 tu ya mapato kwa siku hiyo. Watu wanashindwa kutuma taarifa za nyakata, mizigo inalundikana na gharama zinapanda," alisema Bw. Igogo.

  Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati tatizo hilo kama alivyofanya kwenye suala la TICTS ili kuhakikisha eneo hilo linakuwa na umeme muda wote." Rais asipokee tu ripoti kutoka kwa wasaidizi wake,wanaweza kumpa maelezo yasiyo ya kweli, afuatilie suala hili kama alivyofanya kwenye TICTS ili tupatikane ufumbuzi wa kudumu," alisema Bw.Igogo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 85,194
  Likes Received: 60,492
  Trophy Points: 280
  Hivi kazi za Raisi ni hizi kweli????????????????
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,487
  Likes Received: 1,851
  Trophy Points: 280
  TRA ni kikwazo kikubwa cha uwekezaji,biashara na hasa kama una imports bidhaa utajuta kuzaliwa tz!matatizo hayaishi tra longroom matokeo yake kuwapa watu mzigo wa storage!
   
Loading...