Wadau anaye soma IT soko lake LA ajira lipo vipi

Dah kwa usawa huu... bi mkubwa akikupa hela ya kula bana bana ukimaliza ukafungue kibandaa haina jinsiii
 
Serikali hivi karibuni imekua ikitangaza ajira nyingi za IT japo katika interview zake mahudhurio ni makubwa sana ikidhihirisha uhitaji wa ajira ni mkubwa sana. Mfano. Position ya IT wanahudhuria waliosoma Comp science, IT, Comp Engineering, Telecom eng, electronics & telecom na course kama izo. Private sector nako si tofauti sana. Kikubwa kama unapenda IT kasome, hakikisha unatoka vizuri.
 
Infomation techonology

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi napenda kuwashauri vijana wenzangu tuache kuyapa nafasi mawazo ya kuajiriwa lazima tusome kitu chochote ambacho uki graduate unaweza kuji involve katika kitu ambacho kitaendesha maisha yako bila kutegemea kuajiriwa,yes ajira zikitoka kajaribu ku apply ila lazima uwe umejiajiri somewhere unafanya kitu fulani ku earn income.

Katika utawala wa JK naweza kusema Vyuo viliongezeka sana,uelewa wa watu nao ukaongezeka watu wakaanza kuwapeleka wanafunzi shule nzuri kuhakikisha wanafaulu vizuri hivo ufaulu nao ukawa mkubwa.

Ntakupa mfano mdogo tu,watu wamesoma Doctor of Medicine 5yrs,course ambayo watu wengi walifikiri ina uhaba wa watu hivo wengi kukimbilia huko ila wakasahau katika utawala wa kikwete Vyuo vinavyotoa hiyo course viliongezeka kuanzia namba mpaka intake nayo ikaongezeka kwa hiyo unakuta kwa mwaka wakawa wanatengenezwa madaktari 1,000 ambayo ni idadi kubwa sana kushinda sekta binafsi na serikali kuweza kuajiri wote.

Kinachoendelea sasa ni kwamba degree ya udaktari nayo inaanza kuwa kitu cha kawaida sana mpaka watu wanakosa kazi wanaamua kujitolea bure mahospitalini...Kama una ndugu au rafiki alomaliza hiyo course between 2014-2016 muulize akupe experience ajira zilivokua shida.
Nacho jaribu kukwambia kwamba zama za kuajiriwa zinaisha hivo...Wasomi wa degree ya kwanza wamekua wengi na wachache wao either walotusua wakiwa chuo au wenye unique capabilities ndo always watakua selected katika hizo ajira.
Struggle for existence and survival of the fittest.

what a beatiful course kama IT unaweza kuanza na computer yako na internet na ukaanza ku earn living kuna kazi mtandaoni huko nyingi katika websites kama Freelancer.com kuna watanzania wengi nao wanataka kufanyiwa kazi zinazo involve hiyo taaluma.

Fungua akili nenda chuo kasome na hakikisha una graduate ukiwa productive ukikosa cha kukupa pesa ni uzembe wako!
 
Back
Top Bottom