Wadaku wa CCM na Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadaku wa CCM na Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Shiefl, Jan 3, 2011.

 1. S

  Shiefl Senior Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanabidii,

  Ikiwa mara yangu ya kwanza kuchangia katika jukwaa hili kuhusu hili suala la katiba naomba niseme kuwa kuna mamluki wa CCM sasa wameamua kuiteka hoja ya katiba mpya. Kama walivyoelezea viongozi waandamizi wa CHADEMA, Tundu Lisu na Dr Slaa kuna watu wameamua kuleta hoja za CHADEMA ni wale wale na kuunga mkono commision ya JK ambayo itakuwa ni kama za marais wa CCM ambao ni wasanii wakuu wa nchi hii. Kama siyo CCM mtanzania asingekuwa wa tatu kutoka mwishoni kwa kipato Africa.

  Hivi sasa mafisadi nao wanashangilia hoja ya Katiba mpya wakijua sasa media yote itahamia kwenye hii topic ambayo msanii wao mkubwa ameshaamua kuidandia.
  Ni bora watanzania tukakalia hoja ya msingi ya kuanzishwa mjadala wa kitaifa si mambo tume ambazo tumeshazoea ni uhuni wa kutafuna pesa za maskini walalahoi wa Tz. Ningefurahi raisi angeunda kamati ya watu wawili au watatu wakawachambua waliotuingiza mkenge wa kutaka kulipwa Dowans ili wakalipishwe lile deni badala hawa wadanganyika maskini kuporwa zao kidogo kupitia ongezeko la bei ya umeme hivi sasa.

  Kwa taarifa yenu mkuu kaona Kijana mwanyika atajipatia umaarufu, so akaamua na yeye akaunde katiba ili sifa zimjie juu yeye bwana wa masifa. Yani sijui tumelaaniwa na siye wadanganyika.

  Ah, wacha niachie hapa maana sasa inatia uchungu Tz yangu inaelekea wapi?
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Pole mkuu usijali na 2015 CCM watapeta pamoja na hali mbaya ya wabongo...
   
Loading...