Wadaiwa wa HELSB ukiacha kazi Mafao hupewi NSSF.. wanakata deni lao

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
habari wadau..

Jamaa yangu amerudi ofisini na manung'uniko tele.. alikuwa na mradi wake alipanga mwezi ujao aache kazi kisha achukue mafao yake akawekeze kwenye biashara yake zaidi ajiajiri..

sasa ameenda nssf kucheki utaratibu... kaambiwa kama unadaiwa na bodi ya mikopo.. cheque yako itabuma tu...

maana helsb watakata chao juu kwa juu chote..

hapo jamaa ana milion 16 nssf, na heslb wanamdai milion 11... si majanga haya...

bora mlioacha kazi zamani
 
safi sana. dawa ya deni ni kulipa. ni kwa mifuko yote. yani penye pesa HESLB wamepenyeza wakala wao (Credit Info), hamna kuchomoka!
 
Wakati anatumia hela za bure alikua anaona raha sasa hatakiwi kunung'unika atulie dawa imuingie
 
Pamoja kwamba dawa ya deni ni kulipa lakini sio sahihi kukata pesa ya mtu kwa mkupuo kana huyo mtu amegoma kulipa kidogo kidogo.
 
Nafikiri bodi ya mikopo inabidi wajipange namna ya kukusanya madeni bado hawana mfumo mzuri. Hii bado sio njia sahihi, tatizo sio kwamba watu hawataki kulipa tatizo wanalipaje.. So kuna tatizo sana huko kwao.
 
habari wadau..

Jamaa yangu amerudi ofisini na manung'uniko tele.. alikuwa na mradi wake alipanga mwezi ujao aache kazi kisha achukue mafao yake akawekeze kwenye biashara yake zaidi ajiajiri..

sasa ameenda nssf kucheki utaratibu... kaambiwa kama unadaiwa na bodi ya mikopo.. cheque yako itabuma tu...

maana helsb watakata chao juu kwa juu chote..

hapo jamaa ana milion 16 nssf, na heslb wanamdai milion 11... si majanga haya...

bora mlioacha kazi zamani

halafu ukute hata chuo alikua hali boom lote anamhonga jane!!..leo hii jane anakula good time na mumewe yeye anatembea na mafomu ya NSSF mjini
 
Nafikiri bodi ya mikopo inabidi wajipange namna ya kukusanya madeni bado hawana mfumo mzuri. Hii bado sio njia sahihi, tatizo sio kwamba watu hawataki kulipa tatizo wanalipaje.. So kuna tatizo sana huko kwao.

kwani mtu akikukopesha wakati wa dhiki utasubiri aje kukugongea mlango ili umlipe pesa yake?? watu waende bodi kulipa deni badala ya kukimbilia kununua magari.. watu wakishaajiriwa wanasahau na hawataki kulipa deni dawa yake ndio hiyo!..lazima tuwe na discipline ili wadogo zetu nao wasome
 
Dah ni shida!, tumeliwa. nilikuwa na kampango kama hako, sasa ngoja niache kazi mapema ili nijiongoze mwenyewe tu!. Wanabana kote kote, na viajira uchwara hivi vya Tanzania kweli tutapona? au wanataka wote tujazane serikalini huko tuwe tunaiba. Umenifungua macho ndugu yangu, NSSF wamenila sina changu tena, wenye roho nyepesi tunahamia PLAN B maana A inadalili zote za kufeli
 
Hivi ulitaka usomeshwe bure ile HELSB imekuwa ndo mzazi wako ili ukimaliza kusoma ndo utokomee na pesa za wavuja jasho ,,, ndo raha ya panga la mkopo ni tamu kwao Ila kanauma upande wa pili
 
wanatumia nguvu nyingi kwa kukwepa kutimiza wajibu.

Graduates wote wapo, Hadi wanaweka pesa NSSF/PPF etc maana yake waajili wanajulikana.
Ikipitishwa sheria kuwa Kila mwajiri ni Sharti kupeleka majina ya wafanyakazi wake wote HSLB, na HSLB wakawa na SYSYTEM ya kufanya mapping kati ya Database yao na majina hayo, Watakamata wadaiwa wote ndani ya siku mbili na kuanza kukatwa pesa. Au Hakuna aliyeajiliwa/jiajili asiye na account bank, HESLB ikifanya mapping ya hawa wadaiwa majina yao na account za benk watawapata hadi wale wanaojifanya wanabiashara zao.


Kwa kufanya hivyo watakusanya pesa nyingi kwa mpigo huku zikiwasaidia watu wengi kwa wakati. Ukitegemea Mtu astaafu au Aache kazi kabla ya umri Uvizie kipato chake cha kujikimu, utakuwa umeamua kuchota maji kwenye bomba linalotoa Matone huku ukiacha Option ya kufungua bomba lote.


Narudia Huu ni ukomo wa ubunifu huku ukiwa na rasilimali zote za kuwabana watu. Lengo sio kuwafirisi wadaiwa ila ni kuwafanya watoe kwa wakati.

Siungi mkono mtu kukimbia Ila pia sio sahihi kumkopesha mtu mamilioni bila kujua hatayarudishaje au hayarudishe kwa hiyari yake wakati dunia imejaa SYSTEM rahisi kabisa kuwafanya wote wenye KUpenda na Wasiopenda Kusudisha mikopo yao Wanarudisha.
 
Huo ni uongo aende bodi watampa utaratibu....kwanza si sheria ...unaenda bodi unaeleza kwamba unaacha kaz unapatikana wapi na dem lao unalipaje only
 
Back
Top Bottom