singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
HATIMAYE Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetoa siku 60 kuanzia juzi kwa wanufaika wa mikopo wanaodaiwa wajitokeze ili kuanza kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua.
Katika muda huo uliotolewa, waajiri pia wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza wajibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu katika vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Agizo hilo la bodi si la kwanza bali ni mwendelezo wa maagizo mengi yaliyowahi kutolewa kabla.
Kwa maana nyingine ni kwamba, mara zote ambazo bodi hiyo imetoa mwito kwa wahusika kulipa madeni yao, wamekuwa wakikaidi kulipa na huenda hata ndani ya siku 60 zilizotolewa safari hii wataendelea kupuuza.
Hizi si habari njema kwani inatia aibu kuona Watanzania waliowahi kunufaika na mikopo hiyo kutoka serikalini na leo wamegeuka kuwa wasaliti wa Watanzania wengine wanaostahili kunufaika na fursa hiyo pia.
Kilio cha wanafunzi wanaoshindwa kulipa ada za vyuo nchini kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka, kutokana na wengi wenye sifa kushindwa kupata mikopo hiyo kutokana na uhaba wa fedha, hivyo wakati mwingine kupoteza fursa hiyo muhimu kwa mustakabali wa maisha yao ya baadaye.
Ukubwa wa tatizo hilo ndio uliomfanya Rais John Magufuli wakati akifanya kampeni za kuingia Ikulu, kuichukua ajenda ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuwa ya muhimu, kwa kutoa ahadi ya kuishughulikia kumaliza urasimu katika utolewaji wake.
Ili kuonesha kuwa azma yake ya kupambana na urasimu huo, mara baada ya kuingia madarakani amehakikisha anafuatilia, ambapo hivi leo idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo hiyo imeongezeka na kuleta faraja kwa walengwa.
Kwa maoni yangu, pamoja na kusifu hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kupanua wigo wa wanufaika wa mikopo hiyo, sioni kama ni sahihi kwa wahusika waliowahi kunufaika na mikopo hiyo kutojitokeza hadi sasa ili kulipa madeni yao.
Kama nilivyosema awali, ni jambo la kusikitisha kuona kuwa watu ambao walinufaika na mikopo hiyo wanageuka kuwa wasaliti wa mfuko huo. Hili si jambo la kizalendo hata kidogo na ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe mara moja kwa wahusika wote ili walipe na kuufanya mfuko huo uweze kutoa mikopo kwa wengine.
Inawezekana zipo sababu kadhaa za msingi kwa baadhi ya wanufaika kushindwa kulipa madeni hayo, lakini nionavyo mimi, wengi wa walionufaika wanasumbuliwa na jinamizi la ubinafsi tu, ndio maana hawataki kulipa madeni ili kuwanufaisha wengine.
Utafiti unaonesha wengi wa wanufaika walioshindwa kulipa, wanashikilia nyadhifa mbalimbali serikalini, katika mashirika ya umma, mashirika ya kimataifa na kwenye sekta binafsi. Kwa maana nyingine, watu hao ambao hawalipi madeni ni watu ambao leo hii wana uwezo mkubwa kifedha.
Kutokana na hatua hiyo, ninasisitiza kuwa ni lazima wahusika wote walipe madeni yao ndani ya siku 60 zilizowekwa na bodi hiyo na baada ya hapo kusiwepo na huruma ya aina yoyote kwa atakayeshindwa kutekeleza hilo.
Ni jambo la kupongeza kuona kuwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa, lakini ni lazima hatua hizo ziende sambamba na meno makali ili wahusika watakaokaidi agizo hilo wawe mfano kwa wenzao wanaodhani kuwa fedha hizo za mkopo ni sawa na kichwa cha mwendawazimu ambacho yeyote