Wadada wavaa mawigi na kutingisha vichwa vyao kidogo pindi uwaongeleshapo..

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
735
Kumekuwa na ka tabia ka hawa madada zetu wanao jiweka mawigi vichwani mwao halafu ikitokea unaongea nae basi anajifanya kutikisa kichwa hivi huku akiweka sawa hizo nywele zake bandia..

Kwa mda mrefu nlikuwa sijaelewa kwanini wanafanya hivo ila baada ya mda kupita nimegungua hasa baada ya kuwaona wazungu wakifanya vile nikagungundua kuwa hata hawa dada zetu wamekuwa wakifanya vile ili kujifananisha na wazungu kwani kuna mda unakuta mdada anatikisa kichwa wakati hizo nywele bandia zake wala hazijakaa vibaya kisa swaga za kizungu.

Nimejiuliza maswali hivi na wazungu nao wana mawigi ya nywele vipilipili kama zetu? Kwa sababu kama ni kuwatukuza wazungu tumezidi ikiwezekana tupunguze kidogo kwa sababu licha ya hayo manyele ya amrehemu unakuta mdada mweusi huku kwetu ushenzini kajichubua ngozi yake na mavipodozi ili awe mweupe kama mzungu.

Ombi langu kama mtu mweusi kutoka huku weusini tupunguze kuwatukuza hawa wazungu kwani inafika mda tunamkufuru hata muumba wetu kwa kujibadilisha vile alivyotuumba na kutaka tuwe, siku ya mwisho atasema ww nilikuumba weusi na nywele kipilipili mbona leo upo hivi? Kwa sabab mungu ameumba kila kiumbe kwa sabab maalumu..

Sasa ni nini kifanyike ili kupunguza hali hii kwa watu wetu ili tujivunie na sisi tamaduni zetu ili siku moja zisiwe tamaduni za kishenzi ?
 
Mkuu katika ulimwengu huu Muafrika na Mzungu wanaongoza kwa umburura:-

1 Mzungu anachomuiga muafrika:- Makalio,Maziwa,Lips na Tanning(kufanya ngozi yao iwe brown)
2 Muafrika anachomuiga mzungu:- Mkorogo,Mavazi,Nywele bandia,Lugha(Mtanzania akijua english anajiona ameshakuwa kama Bill Gates) kumbe muuza nyanya wa kariakoo
 
Kuna Kitabu cha Things fall apart or song of Lawino mimekikumbuka

Kuna Dada alikuwa na Nywele Kipilipili lakin akiongea anaiga style ya Madada wa Kizungu ambao wakiongea hutikisa Kichwa Mara kwa mara kurekebisha Nywele zinazozonga usoni kwa wingi
 
Kumekuwa na ka tabia ka hawa madada zetu wanao jiweka mawigi vichwani mwao halafu ikitokea unaongea nae basi anajifanya kutikisa kichwa hivi huku akiweka sawa hizo nywele zake bandia..

Kwa mda mrefu nlikuwa sijaelewa kwann wanafanya hivo ila baada ya mda kupita nimegungua hasa baada ya kuwaona wazungu wakifanya vile nikagungundua kuwa hata hawa dada zetu wamekuwa wakifanya vile ili kujifananisha na wazungu kwani kuna mda unakuta mdada anatikisa kichwa wakat hizo nywele bandia zake wala hazijakaa vbaya kisa swaga za kizungu.

Nmejiuliza maswali hivi na wazungu nao wana mawigi ya nywele vipilipili kama zetu? Kwa sababu kama ni kuwatukuza wazungu tumezidi ikiwezekana tupunguze kidogo kwa sababu licha ya hayo manyele ya amrehemu unakuta mdada mweusi huku kwetu ushenzini kajichubua ngozi yake na mavipodozi ili awe mweupe kama mzungu..

Ombi langu kama mtu mweusi kutoka huku weusini tupunguze kuwatukuza hawa wazungu kwani inafika mda tunamkufuru hata muumba wetu kwa kujibadilisha vile alivyotuumba na kutaka tuwe, siku ya mwisho atasema ww nilikuumba weusi na nywele kipilipili mbona leo upo hivi? Kwa sabab mungu ameumba kila kiumbe kwa sabab maalumu..

Sasa ni nini kifanyike ili kupunguza hali hii kwa watu wetu ili tujivunie na sisi tamaduni zetu ili siku moja zisiwe tamaduni za kishenzi ?
Daaah...aisee una moyo mgumu

Ngoja waje umwagiwe povu hadi uzimie

Mimi pia wananishangaza sana hao wanaoiga wazungu na kutikisa kichwa kama kuku wenye videri

Na usiombe hilo wigi linyeeshewe...hiyo harufu ni balaa
 
Nimekumbuka kadhia iliyomkuta Naomi Campbell

0479cc75efa50277cf436979e7cabd6b.jpg

a55c07c038c03ce11b55c47b743dab93.jpg
 
Haohao wavaa mawagi ndo mnawapenda msivunge hapa.
Yaani wanaume wa Jf wananishangaza... Wasichana wanaowaponda huku, wakienda mitaani ndo wanawakimbiza... Mdada akijisukia zake twende kilioni a.k.a mnyoosho wanamuona mshamba. Alafu huku wanalalama kutaka wadada natural!!!
 
Binafsi napenda natural hair
Kama ni wigi (kwa wale ambao hawajabahatika kuwa na Nywele ndefu) liwe Kama Nywele za asili na Sio makatani yaliyo pakwa rangi
Huo ni mtazamo wangu binafsi
 
Yaani wanaume wa Jf wananishangaza... Wasichana wanaowaponda huku, wakienda mitaani ndo wanawakimbiza... Mdada akijisukia zake twende kilioni a.k.a mnyoosho wanamuona mshamba. Alafu huku wanalalama kutaka wadada natural!!!
Huyo wa twende kilioni, mabutu au tatu kichwa mimi ndio namtaka huyo.

Sijawahi kupenda hizi katani nyeusi kwa wadada.
 
Yaani wanaume wa Jf wananishangaza... Wasichana wanaowaponda huku, wakienda mitaani ndo wanawakimbiza... Mdada akijisukia zake twende kilioni a.k.a mnyoosho wanamuona mshamba. Alafu huku wanalalama kutaka wadada natural!!!

Ukiona Mtu anakufukuzia Pengine kapagawa na Tako au Lips au Mguu Wewe unadhani Hilo Fuko la kufunika Kichwa ndio linalokuuza!

Haiwezekani Nizuzuke kwa ajili ya Hiyo mifuko ya Kichwani ambayo kabla ya kuanza Heka heka lazima uivue ubaki na Kipilipili

Wadada wengi Tatizo lao hawajui their Key successful factor!
 
Why is this even up for discussion ? I don't mind if you got a weave or extensions as long as you look fine...ladies keep doing your thing and keep that swag on a hundred !
 
Back
Top Bottom