wadada wa kileo hivi vazi la suti kwa wanaume linawavutia?

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,532
1,124
leo bataka nipate mtazamo wa wadada huhu kuhusu hili vazi maarufu duniani?

je mnalipenda livaliwe na wapenzi wenu?

je linawavutia?

wanaume pia mtakuwa na majibu toka kwa wapenzi wenu .ila mimi sijawahi ombwa kutinga suti na mamaa
 
Mh me hata sipendi avae suti anavaa suti kwa minajili.ya kwenda wapi?? Avae simple tu inatosha
 
Sitaki kabisa avae huo mjumba.
Kwanza wanaume wanaovaa suti, mara nyingi huwa wana matatizo ya kunuka miguu....:peep:
 
Zinazotengenezwa na sheria Ngowi yes , siyo zile za Kariakoo zinabana kama skintight na kuvuta eneo la kati juu huku miguuni ikiiimba dont touch my shoes!
 
Sitaki kabisa avae huo mjumba.
Kwanza wanaume wanaovaa suti, mara nyingi huwa wana matatizo ya kunuka miguu....:peep:

haahahha...wewe utakua unakutana na wanasheria maana wanzungukiaga kwa miguu hizi mahakama hapa town mchana kutwa....kweli lazima wanuke miguu. Na zile suti nyeusi huwa wanapata shida sana...ila hawana jinsi maana ndio sharia lazima wavae.
 
hapo madam B umenena kwanza vimiguu hutoa tuharufu sababu muda mwingi hufungiwa kabatini

Yaani utakuta mtu kavaa chupi, boksa, lipensi, suruali ya kitambaa halafu juu anavaa suruali ya suti.

juu ana vest, tisheti, halafu anatupia mkoti.

ukienda miguuni anavaa soksi mbili, moja imetoboka moja nzima, halafu kiatu.
.....sasa pata picha na joto la Dar....halafu atanue kwapa .....:peep: :peep:
 
haahahha...wewe utakua unakutana na wanasheria maana wanzungukiaga kwa miguu hizi mahakama hapa town mchana kutwa....kweli lazima wanuke miguu. Na zile suti nyeusi huwa wanapata shida sana...ila hawana jinsi maana ndio sharia lazima wavae.

Kwani si wavue makoti wakiwa maofisini huko

Yaani Suti hizi...
 
Swali hili ukiwauliza wanawake wa Dar au mji ufananao na huo tegemea majibu ya ajabu ajabu...pia wasio na ujuzi wa elimu ya mitindo watakupa majibu ya juu juu tu.

Lakini njoo downtown NewYork au London na ni wakati wa Fall au Winter halafu uliza swali hili kwa wanawake wa huko, bila shaka majibu yatakuwa tofauti...

Btw kuna namna nyingi za uvaaji suti, huwezi kuniambia mwanamke hakoshwi na uvaaji suti wa mtu kama David Beckham, Guardola, Sheria Ngowi, Clooney etc...
 
sheria ya suti lazima uwe na pesa na usafili wa maana..sio unavaa suti unatembea mitaani vumbi mpaka kwenye ugoko...ila sitaki avae suti mwezangu..anafika mwili mzima mi jasho hewa ya ndani zito kutokana na kushindilia minguo na joto hili la dar....valia simple tu imladi upendezee...sio misuti kama msimamizi wa halusi ahaaaa..
 
Yaani utakuta mtu kavaa chupi, boksa, lipensi, suruali ya kitambaa halafu juu anavaa suruali ya suti.

juu ana vest, tisheti, halafu anatupia mkoti.

ukienda miguuni anavaa soksi mbili, moja imetoboka moja nzima, halafu kiatu.
.....sasa pata picha na joto la Dar....halafu atanue kwapa .....:peep: :peep:
hahahahahah hapa umezidisha chupi, boxer, pensi, suruali ya kitambaa afu ya suti tena hahahahahahahaah sipati picha mtembeo wake anavyo tanua miguu.
 
hahahahahah hapa umezidisha chupi, boxer, pensi, suruali ya kitambaa afu ya suti tena hahahahahahahaah sipati picha mtembeo wake anavyo tanua miguu.

.....utadhani katoka kufanyiwa operation ya busha.

ila serious, nilishawahi kwenda kulala na mbaba flani hivi, alivaa suti....yaani sikuamini kama nguo zote zilitoka mwilini mwake
nahisi alihamisha duka kariakoo akalivaa mwilini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom