Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

neggirl, kwanza sorry for my late reply...busy busy busy!!.

Kuhusu saga la nywele zako (dred rocks) nimekusoma na nimekuelewa.
Ushauri wangu kwako ni huu -:

Fumua dred zako na uanze kuzijenga upya...kwani nikikusoma between the line nagundua siku ya kwanza ulipozitengeneza hawakukata size kubwa ya nywele yako na badala yake walikata vi size vidogo vidogo which is not good and not professional.
Raha ya dred ni lile butu kuwa size ya kati( isiwe ndogo sana na isiwe nene sana). So kama kweli wewe ni mpenzi wa dred na unataka uonekane vizuri ningekushauri ufumue au ukate upya hizo nywele zako na zisubirie kwa miezi mitatu ziote vizuri kisha uanze upya kwa kufuata ushauri wangu hapo juu.

Note: Nenda kwenye professional salon na siyo ilimradi salon.
 
Last edited by a moderator:
Ni cosmetics zipi naweza tumia ili niweze kuwa na rangi moja mwili mzima.? maana jua kali limenitofautisha rangi mwilin.

Fanya mazoezi mara mojamoja upatapo mda na kula matunda kwa wingi hasa baada ya lunch na dinner.

Au kama mfuko wako unaruhusu tembelea kwenye any professional salon au beauty polour na wakufanyie Full facial steamer body scrub.
 
Nimekufatilia kwa muda katk uzi wako huu na hakika unastahil pongezi! mm ni me lakn nafikir unaweza kunisaidia pia kwenye tatizo langu. FUNGUSI ZA MIGUU! Nikivua kiatu hata nzi anakufa! Nitumie dawa gani kwa matokeo ya haraka?

Ahsante sana!!...na pole kwa tatizo lako.

Je,tatizo lako ni la mda gani? Na je umewahi kwenda hospital yeyote?
Karibu tuendelee.
 
Mimi nina tatizo la kuwashwa ngozi ya kichwa hapa kwenye utosi na hakuna mba, nikisuka siwezi kukaa na nywele zaidi ya wiki nawashwa sana na hapo nakua nilishaosha kichwa na kupaka mafuta kwenye ngozi kabla ya kusuka
Unanisaidiaje?
 
Ukiweka curly katika natural hair inachukua muda gani kurudi katika hali yake ya kawaida
 
Ahsante sana mamy kwa response nzuri. Mimi nina maswali kadhaa. Kuna ile style ya kutengeneza nywele na artificial dreads, yaani sijui wanasukia au wanaatach vp hizo artificial dreads, hua wanatengeza kwa sh ngapi? Mimi nipo mwanza. Halafu hizo dreads zinauzwa readymade madukani? How much? Na ukienda dukani unaulizia kwa jina gani? Brand ipi ni nzuri? Ukishatengenezwa unakaa nazo kwa muda gani? Vp matunzo yake?
Sorry kwa maswali mengi, ila I trust you are a professional. Shukrani.
 
Nina ndugu yangu wa kike hua anatoa harufu sana kwenye nywele. Afya yake ni nzuri na hua ni msafi ila tatizo lake ni hilo tuu. Hiyo imemfanya hata asitake kusuka wala kutengeneza nywele, hua anakata tu ili aweze kuziosha mara kwa mara. Yaani akitoka tuu kuoga na kukausha maji na kupaka mafuta kichwani, baada ya dakika 10 harufu inaanza kusikika. As a professional naamini umekutana na wateja wenye tatizo hili labda. Unamsaidiaje ndugu yangu? Ahsante.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom