Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

Mimi nywele zangu ni ndefu hazikui tena natumia movit relaxer dawa ya nywele na steaming lorys sababu nina nywele nyingi kichwani

Mpenzi,sasa kama una nywele nyingi kichwani si ndio vizuri? Si unaona hapa wenzio waliowengi vilio vyao vikubwa ni kukatika nywele kila kukicha? Kuhusu kutokukua au kutokuongezeka...nafikiri ungezitream ki professional ili ziwe level na uenda zitaongezeka kwa urefu.
 
nywele zangu kavu na hazishiki dawa na zinakatika, nilikuwa naweka easy wave sa hivi natumia miadi dawa,mafuta na steaming lakini bado kavu na zinakatika na n brown sana.pia ngozi ya kichwa inauma hata kama sisuki tatizo nini?
 
Ukikata ncha za nywele' kwanza zinakuwa smart,mwenyewe unaonekana smart na pia uenda nywele zako zikaongezeka urefu.

MillionHairs ni mafuta gani ukipaka kwenye nywele zinavurugika vurugika??!Napenda sana hiyo style... na je ni lazima nywele ziwe natural au hata zilizokuwa relaxed zinafaa?!
 
Last edited by a moderator:
MillionHairs ninahitaji kujifunza kutengeneza nywele na ubunifu mbalimbali.
ila siyo kusuka .
ni wapi nitaweza kusoma kozi ya muda mfupi
?
kwa vitendo yaani saloon.
 
Last edited by a moderator:
nywele zangu kavu na hazishiki dawa na zinakatika, nilikuwa naweka easy wave sa hivi natumia miadi dawa,mafuta na steaming lakini bado kavu na zinakatika na n brown sana.pia ngozi ya kichwa inauma hata kama sisuki tatizo nini?

Labda una very sensitive head skin...sasa,kwavile sijaziona hizo nywele zako sitaweza kukuambia chochote. Ila ushauri wangu kwako tafuta any professional hair salon na uwaeleze hilo tatizo lako...tafadhari usiende kwenye vi salon vya uchochoroni hautaambulia chochote zaidi ya longolongo.
 
MillionHairs ni mafuta gani ukipaka kwenye nywele zinavurugika vurugika??!Napenda sana hiyo style... na je ni lazima nywele ziwe natural au hata zilizokuwa relaxed zinafaa?!

Hiyo inaitwa Rough Hair Style...inapendeza na kufaa kwenye nywele kuanzia inch 2 hadi 4 no matter iwe natural au relaxed.
Ni hair style ya kukaa kichwani wiki moja tu...na ndani ya hiyo wiki moja nywele zako usiziogeshe maji. Nakuwekea picha ya product yake hapa chini.

image.jpg
 
Napenda kunyoa, ila nmechoka style moja ya nywele fupi, nifanyeje kufanya muonekano bomba zaid

Jibu lake ni rahisi sana like ABC...acha nywele zako zikue hadi kufikia inch 8 au 10 then utaanza kwenda salon na utafanyiwa style tofauti tofauti kama ulivyokuwa zamani. Ila kama hautojali naomba uniambie hiyo nywele yako kwa sasa ni inch ngapi?
 
MillionHairs ninahitaji kujifunza kutengeneza nywele na ubunifu mbalimbali.
ila siyo kusuka .
ni wapi nitaweza kusoma kozi ya muda mfupi
?
kwa vitendo yaani saloon.

Sawa nimekusoma mpenzi, kuna chuo kimoja kiko hapo maeneo ya Makumbusho jirani na Sayansi ila kusema ukweli sikijui na sijawahi kufika...ningekushauri utafute hicho chuo ili ujue utaratibu wake.

Kuhusu kujifunza kwenye Salon ushauri wangu ni huu:- kama ilimradi Salon basi nenda maeneo ya Sinza,Mwenge,Ilala na Kinondoni...ila kama unataka kujifunza ile silias kabisa basi tafuta Professional salon maeneo ya Posta,Masaki,Mikocheni na Mbezi beach' ukifanikisha kupata moja ya Salon kutoka maeneo hayo na wakakufundisha kitu basi na wewe utakuwa Professional hasa.
 
Ni cosmetics zipi naweza tumia ili niweze kuwa na rangi moja mwili mzima.? maana jua kali limenitofautisha rangi mwilin.
 
Nimekufatilia kwa muda katk uzi wako huu na hakika unastahil pongezi! mm ni me lakn nafikir unaweza kunisaidia pia kwenye tatizo langu. FUNGUSI ZA MIGUU! Nikivua kiatu hata nzi anakufa! Nitumie dawa gani kwa matokeo ya haraka?
 
Back
Top Bottom