Wadada na Magari

A-town

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
494
169
Nimejaribu kufuatilia sana na sasa naweza kusema kwa yakini kuwa kina dada wengi wanamuona mkaka mwenye gari kuwa ndiye alieyapatia maisha.

Hii haijalishi kiwango cha elimu cha mdada wote wanatazama gari kama kigezo kikuu cha mafanikio kwa mkaka.

We uwe na majumba na vitega uchumi kibao kama hutembelei gari mbele ya macho ya wadada unaonekana kama mtu aliyefulia kimaisha.

Nimejaribu kuwahoji hata baadhi ya wadada,wale waliokubali kuzungumza walifunguka wakisema wadada wengi wanapenda kula bata na gari ndio kitu pekee kinachowezesha ulaji wa bata kwa urahisi hivyo gari ni muhimu kuliko vingine.

Karibuni kwa mjadala.
 
huo utafiti uliufanya kwa wadada wa wapi na wenye kiwango gani cha elimu, na umri gani?
 
Siwafichi hakuna kitu ninachochukia kama kuendesha gari,nahisi labda kutokana na hizi changamoto za foleni,na si kuendesha tu hata kupanda basi.napenda baiskeli na pia pikipiki au bora nitembee na miguuu
 
Wadada si tu wanapenda mtu anaemiliki gari lake hapana...Yaani wewe ukiwa una-drive gari hata liwe ni lakampuni baadhi ya wadada wako tayari kukupa ama kufanya chochote na wewe...Shida kubwa baadhi ya hawa dada zetu wanapenda maisha ya kutambiana na maigizo kisa tu rafiki yake ana-boyfrnd mwenye gari na yeye atahakikisha anapata mwenye gari na ukimpa lift hatoshuka atakuomba hadi umfikishe nyumbani kwao ama mahali wenzake watamuona sasa wakati anaku-convice ndiyo mwanya huo wanaume wakware hutumia kumweka kwenye himaya yake....Maana hawezi kataa chochote..
 
Hao madem njaa na elimu ndogo perhaps kukulia maisha ya dhiki sanaa. Wanaojielewa hujua ni vitu minor sanaa hvyo.

Alaf wengi wao wadananda sanaa.
 
huo utafiti uliufanya kwa wadada wa wapi na wenye kiwango gani cha elimu, na umri gani?
kwahiyo unamaanisha wenye elimu kubwa hawashoboki na magari???......ushobokeaji wa gari hauhitaji kiwango cha elimu alichonacho mdada na kama yupo mdada asiyependa gari mlete tuone!
 
Niliwahi kuishi na mdada aliyekuwa akifanya masters TUMAINI alichanganyikiwa na mkaka aliyekuwa akiendesha gari la Voda. Yani alikuwa akikaa mbele na miguu kwenye dashboard huku gari nje lina charter ya Voda anaona maisha yamekamilika.
 
Hao madem njaa na elimu ndogo perhaps kukulia maisha ya dhiki sanaa. Wanaojielewa hujua ni vitu minor sanaa hvyo.

Alaf wengi wao wadananda sanaa.

Wengi wao tamaa tu ya maisha mazuri wakati wanakotoka hali haishawishi kuishi wanavyotaka.
 
Mmoja juzi akatoa kali ya mwaka, kamkaushia mwalimu wake kama hajamuona. Alipoulizwa anajibu eti alikuwa na mtu mwenye wivu mno sasa asingeweza kwenda kumsalimia mwl wake. Yani mwl aliyemfundisha kidato cha tano na sita leo ndio yuko mwaka wa kwanza eti jamaa yake ana wivu sana hivyo alishindwa kushuka garini kwenda kumsalimia mwl wake.
 
Back
Top Bottom