Wadada msioolewa muwalaumu wazungu kudanganya kuhusu ndoa ya mke mmoja

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,495
2,000
Unapokuwa muamini inakubidi kuamini kwa asilimia yote.. Lkn ukiamini au kutokuamin kwa sababu kuna kifungu kinafunua uovu wako au kukataza tamaa zako basi ww si muamini. Mkristo wa ukweli huiamini bible yoteee na hata kilichoandikwa ktk bible si kama mwanadamu alivyopenda na kuona bali waliongozwa na Roho ya bwana katika kila hatua.
tatizo hawa wazungu hawaaminiki ndugu yangu,bible wameicompile wao mi mkristoila nina mashaka na bahadhi ya mambo na sio dhambi,ndio maana hata martin luther akawapinga wakatoliki ikatokea lutheran church other wise dunia nzima kungekuwa na dhehebu moja kama kila kitu kitaeleweka na kutafsiriwa sawa kwa kila muumini
 

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,495
2,000
Una-edit Biblia?
hapana wala sina ubavu huo tunajadiliana je unajua kuwa watu wengi wanaoa mke mmoja na wanamichepuko kadhaa nje ,je ndio mpango wa Mungu,je mpango wa Mungu kuwa dada zetu wapate Ttaabu kusaka ajira pia wapate taabu kusaka mume
 

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,495
2,000
Akiwa na mke mmoja na michepuko miwili tena na wao wana watoto na wanahudumiwa kama wake huo sio uzinzi eeeh?
Honey Faith ndio hali halisi huku mitaani mtu anajifanya ana mke mmoja siku akifa makaburini mnaona vitoto vinafanana na nyinyi pembeni kuna mama analia anagalagala kuliko mke wa ndoa kumbe small house
 

Ledwin

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
225
195
unajua wazungu huwa siwaaminiamini,mwanzo walisema sayari ziko tisa sasa wanasema ziko nane na tunakubali.

Tukija kwenye ndoa agano la kale linaongelea ndoa ya wake wengi ila agano jipya linasema mke mmoja ,nasema hiyo ni idea ya mabepari ili masikini ukioa tu imekula kwako lakini wao(mabepari) kwa kuwa wana uwezo wataoa mke mmoja wakimkinai watachepuka kwa mke wa masikini kama akimvutia,ni ngumu sana mwanamme masikini kuchepuka na mke mke wa tajiri kama ikitokea, na ukikamatwa utauliwa,

hawa wazungu walichakachua hicho kipengele kwa maslahi yao binafsi,kuna amri pia zinadaiwa kuchakachuliwa na wamisionari kama watangulizi wa wakoloni ili kulainisha mioyo ya makoloni(waafrika).

Mimi kama mkristo siamini kama ndoa ya mke mmoja ni agizo la mungu kwani hakuna mwanamume anayetosheka na mke mmoja na idadi ya wanawake ni wengi kuliko wanaume ,hivyo wadada msioolewa muwalaumu wazungu kwa uongo wao.

Makanisa ya kiroho kumejaa mabinti warembo kwelikweli wanaombewa kila siku wapate wanaume wa kuwaoa kisa uongo wa mzungu.
je mke naye akimkinai mume wake ,anaruhusiwa kubadilisha,maana na wanawake nao wanakinai ila wanavumilia tu.
 

nameless girl

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
4,131
2,000
nimeoa mke mmoja ndio lakini we unajua nina michepuko mingapi?ahahahahaha kiding
Tukichukulia utani wa michepuko, ni tofauti sana na mke. Hubebi majukumu yake yote kwa 100%, you choose what to do and what not to...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom