Wadada, Mkisalimiwa Jibuni Salaam, Sio Kila Salaam Ina Ubaya Ndani Yake.

Nilichoandika sio mawazo,ni kitu kipo...mimi ni wa kike,nina marafiki wa kike wenye hizo tabia na wananipa hiyo sababu

Ninae rafiki hakubali salamu ya mwanaume asiye na gari
Kwake yeye mwanaume mwenye gari ndio mwenye haki ya kuongea nae
Unakuwaje na rafiki asiyejielewa kwa kiwango hicho Le dadaz
 
Sema nn kusalimia salimia watu hovyo napo haijakaa fresh . Salimia mtu kma unashida nae au kuna kitu unataka kuuliza

Watu wanashida zao , wengine ma stress kibao jua ni kali na hela hakuna unaweza salimia mtu kumbe yuko mbali kimawazo

Yawezakuwa hata huyo sister alikuwa anamuwaza mgonjwa wake ukiplus amechelewa kupeleka chakula hujui alipotoka yamemkuta nn au anayeumwa n nan

Waza positive zaid masalam salam yanepitwa na wakat utakuja kuwek kinyongo kwa vitu vinavyoepukika tu
 
Mm kuna siku niliamua kwenda kwa kaka yangu aliachana na mkewe sasa kumbe pale kwake alikua kaleta kidem . Mm nimefika nikapiga hodi akanifungulia nikamsalimia akajibu kwa nyodo yaan kijeuri maana sio siri bro yuko vizuri kiuchumi basi dem alikua anaona kila anae kuja pale ni pimbi fulani sikukaribishwa hata ndani akaniuliza una shida na nani nikauliza fulani yupo akasema kalala hataki kusumbuliwa huku akifunga mlango kuna jamaa alikua nje alie nifungulia geti ni family friend alicheka sana mm nikapiga simu kwa broo ..broo akaja kufungua mlango yule dem mm sikusema chochote yule dem alivo itwa kutambulishwa kua huyu ni mdogo wangu wa damu alijisikia vibaya sana ila alijua kabisa kaharibu ile mbaya ..Sijui kwa nn wanawake hua na vizarau bila kumjua mtu.
 
Mkuu huenda hakusikia, sio wote wana tabia hizo.

Au labda alikua na mawazo ya mgonjwa wake na huo mda alofika akijua huenda kachelewa na mgonjwa wake hatopata mlo wa mchana wa siku hiyo.

Kwa mimi naona ulimhukumu bure dada wa watu, na je ulimsalimia zaidi ya mara moja?? Kama sivyo basi we jamaa una kujiskia kwa kijinga na unapaswa kupuuzwa kwa hizi lawama unazomtupia bidada!!

Hahahaha...!
 
Mm kuna siku niliamua kwenda kwa kaka yangu aliachana na mkewe sasa kumbe pale kwake alikua kaleta kidem . Mm nimefika nikapiga hodi akanifungulia nikamsalimia akajibu kwa nyodo yaan kijeuri maana sio siri bro yuko vizuri kiuchumi basi dem alikua anaona kila anae kuja pale ni pimbi fulani sikukaribishwa hata ndani akaniuliza una shida na nani nikauliza fulani yupo akasema kalala hataki kusumbuliwa huku akifunga mlango kuna jamaa alikua nje alie nifungulia geti ni family friend alicheka sana mm nikapiga simu kwa broo ..broo akaja kufungua mlango yule dem mm sikusema chochote yule dem alivo itwa kutambulishwa kua huyu ni mdogo wangu wa damu alijisikia vibaya sana ila alijua kabisa kaharibu ile mbaya ..Sijui kwa nn wanawake hua na vizarau bila kumjua mtu.

Yaaaaani huwa najiulizaga hilo swali lakini sipatagi jibu mkuu.

Yaani wana ulimbukeni flani hivi baadhi yao. Stupid kabisa...!
 
Thanks Nuzulati mi nafkiri hii pia inachangiwa na malezi huko walipolelewa walipewa malezi ya hovyo utakuta.

Coz ukishapewa malezi yalo mazuri toka udogoni unakua ukiwa na tabia njema kwa yeyote utakayekutana nae, ila kama malezi ni ya hovyo basi hata tabia nayo inakuwa ni ya hovyo kabisa.
Na hapo kwenye malezi ndo mzizi mkubwa ulipo
 
Na hapo kwenye malezi ndo mzizi mkubwa ulipo

Haswa mkuu na ukiangalia kizazi hiki cha .com mambo yanazidi kuwa hovyo kwa hawa watoto, wakaka, wadada wa kisasa, wachache sana wapo kwenye maadili mema ila asilimia kubwa iliyobaki mambo yao ni hovyo kabisa kwa kweli...!
 
Wenye dharau wapo na pia kuna muda kichwa kinakuwa kipo hovyo yaani anaongeleshwa kumbe yupo mbali kifikra hali inayopelekea hata asisikie akiongeleshwa/Kusalimiwa.

Huyo dada inawezekana alikuwa mbali kifikra, labda mawazo yake yote yalikuwa kwa mgonjwa aliyekuwa akienda kumuona ama kwingineko.

Muda mwingine tusihukumu sana.
 
Sawa kiongozi ila asilimia kubwa ya hawa viumbe ni wapo hivyo mkuu...!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom